Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utalipa Sh 28,000 kwa mwezi ili kupata Instagram Verification

Insta Verify Utalipa Sh 28,000 kwa mwezi ili kupata Instagram Verification

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya META imetangaza kuwa itaanza kuweka huduma ya kulipia ili kuweza kupata verification badge (alama ya uthibitisho).

Huduma hiyo itakuwa inafanana na ile ya Twitter Blue Tick ambapo watumiaji wataweza kulipia ili kupata alama ya verification na upendeleo wa akaunti kuwa tofauti.

Instagram na Facebook ambazo zote zinamilikiwa na META zitaendelea kupatikana bure, lakini kwa ambao watahitaji Badge ya verification watalipia.

Badge ya verification

Meta itazuia mtu asifungue akaunti kama yako au akaunti za kutumia majina yako

Meta itaweka support ya huduma kwa wateja

Comments yako itaonekana kwa urahisi

Utapata upendeleo wa content zako kuonekana kwenye page ya Explore, Search na Reels

Utapata Stickers maalum kwenye IG Stories.

Akaunti ambayo imelipia verification itakuwa ya mwanzo kuanza kupata mabadiliko mapya kabla hayajaanza kutoka kwa watumiaji wote.

Meta imesema gharama zake zitaanza kuwa Dola 11.99 (sawa na Tshs 29,000 kwa mwezi) endapo kama utajiunga kwa kutumia Website. Kama utajiunga kwa iOS utalipia 14.99 (sawa na 35,000 TZS) kwa mwezi (gharama ambayo imeongezeka ni gharama ya asilimia ya Apple).

Twitter, Snapchat, na Telegram ni moja kati ya apps ambazo zinatumia utaratibu huu!

Je unadhani mitandao kuanza kulipisha watumiaji wake ili kupata huduma za kipekee na verification ni sawa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live