Utafiti mpya umethibitisha kile ambacho wakosoaji wengi wa mapenzi ya mtandaoni wamekuwa wakisema, 'Wapenzi na wanandoa wanaoweka picha na mahusiano yao wazi kwenye mitandao ya kijamii hawana furaha na hutaka ulimwengu uamini wanafuraha na amani'.
Utafiti wa Shotkit wa wanandoa 2,000 umetazama tabia zao mitandaoni, wanachopost na wanavyoishi na umegundua wanao-post zaidi ya selfies tatu kwa wiki wanadaiwa kutokuwa na furaha kwa asilimia 128.
Utafiti umegundua kuwa sababu ya Wapenzi kupost sana kuhusu mahusiano yao ni 'uaminifu kwenye mahusiano' na kutaka kuonyesha watu kuwa wako kwenye mahusiano na mtu flani, asisumbuliwe.