Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Utafiti Unaonesha Binadamu Anapoteza Siku 26 Kila Mwaka Kwa Kutofanya Lolote

Batch Simu Utafiti Unaonesha Binadamu Anapoteza Siku 26 Kila Mwaka Kwa Kutofanya Lolote

Thu, 7 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JE umeshawahi kujiuliza kwa mwaka ni muda kiasi gani unaoupoteza kutokana na kutofanya chochote? Mathalani, mtu anakusubirisha tu sehemu halafu mwisho wa siku hatokei. kimsingi unakuwa umepoteza muda wako bure.

Matukio ya aina hiyo ya kupotezewa muda wako bure ukiyajumlisha kwa mwaka mzima kadri yanavyokutokea unadhani mwisho wa mwaka utakuwa umepotezewa muda kiasi gani?

Majibu ya swali hili yanahitaji utafiti.

Kwa mujibu wa Utafiti uliodhaminiwa na Duolingo na kufanywa na Onepoll umebaini kuwa binadamu wa kawaida anapoteza muda wa mwezi mzima kila mwaka kwa kutofanya chochote.

Utafiti uliofanywa kwa watu 2000 raia wa Uingereza umebaini kuwa binadamu wa kawaida anapoteza muda wa zaidi ya siku 26 kwa mwaka kwa kutofanya chochote, masaa 12 kwa wiki au zaidi ya masaa 624 kwa mwaka.

Kwa zaidi ya nusu ya waliohojiwa wamekiri kwamba kusubirishwa kwenye simu ndiyo jambo linalopoteza muda kwa asilimia kubwa, maana yake ni kwamba mtu anakupigia simu halafu anakuambia nisubiri kidogo! (Anakusubirisha) unapoteza dakika kadhaa kusubiri mtu huyo muda wote huo unakuwa haufanyi chochote kwahiyo muda unakuwa unapotea bure.

Asilimia 45 ya kupoteza muda ni pale unapokuwa umepanga foleni ya kupata huduma kwa mfano Benki, sehemu ya huduma ya maji, hospitali n.k

Sababu nyingine zinazopelekea kupotea bure kwa muda ni kama kukaa kwenye foleni za barabarani ambayo utafiti umeonesha ni kwa asilimia 44, matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo utafiti umeonesha yanapoteza muda kwa asilimia 21 na kusubiri kitu kichemke mathalani maji au chai muda hapo hupotea kwa asilimia 15.

Kusubiri nguo zifuliwe na mashine, kusubiri huduma mgahawani au hotelini na kusubiri bidhaa uliyoagiza ifike (Delivery) vyote hivi vinakula muda. Matumizi ya mitandao ya kijamii

Katika utafiti huo asilimia 47 ya wazee wamesema wanajikuta wanakaa bila kitu cha kufanya takribani mara tatu kwa siku na hiyo inatokana na kukosa hamasa ya kufanya kazi, na kwa nyongeza tu ni kwamba asimilia 56 ya watu waliohojiwa katika utafiti huo wamekiri kuwa wanatakiwa kulifanyia kazi suala zima la matumizi sahihi ya muda.

Katika kupambana na suala la kutunza muda imebainika kuwa asilimia 38 ya binadamu wanapoteza muda wao mwingi katika kuangalia televisheni pamoja na matumizi ya mtandao wa intaneti.

Majibu ya watu waliohojiwa kuhusu nini kifanyike ili kuwa na matumizi sahihi ya muda kwa asilimia 70 wamesema watautumia mwaka huu wa 2022 kujifunza njia na ujuzi mbalimbali ili kuokoa muda unaopotea bure.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live