Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti: Private Jet za mastaa duniani zinavyochafua mazingira

NINTCHDBPICT000714020925 Utafiti: Private Jet za mastaa duniani zinavyochafua mazingira

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti wa hivi karibuni nchini Marekani umebaini Mastaa wanaomiliki ndege binafsi wanashiriki kwa asilimia kubwa kuchafua mazingira kwa ndege zao kutoa hewa ya Carbon dioxide (CO2) kwa kufanya safari nyingi zisizo na ulazima.

Utafiti huo wa Driven Digital Marketing Agency (Yard) umeeleza ndani ya mwaka mmoja pekee Staa mmoja wa Marekani kupitia ndege yake anazalisha tani 3,376.64 za CO2 ambazo ni zaidi ya mara 482.37 za uzalishaji wa hewa hiyo kwa mtu anayetumia ndege za umma ambapo huzalisha tani saba tu kwa mwaka.

Hawa ni Mastaa 10 Marekani ambao wanatumia zaidi usafiri wa ndege binafsi jambo linalopelekea uchafuzi wa mazingira kwa kuzalisha hewa ya Carbon dioxide (CO2).

Taylor Swift

Hadi sasa amefanya safari 170 ambazo ni sawa dakika 22,923 au siku 15.9 alizotumia angani, safari zake ni kama ziara za kimuziki ambapo safari moja huweza kuchukua hata dakika 80 wastani wa umbali wa maili 139.36. Hiyo kwa ujumla amezalisha tani 8,293.54 za CO2.

Floyd Mayweather

Bondia huyu amezalisha tani 7,076.8 za CO2 katika safari zake 177 ambazo ni wastani wa safari 25 kila mwezi, huku ikitajwa safari fupi zaidi ya ndege aliyowahi kuifanya ilitumia dakika 10 tu angani!.

Jay-Z

Rapa huyu amefanya safari 136 ambazo zimezalisha tani 6,981.3 za CO2 ambazo ni zaidi ya mara 997.3 za hewa hiyo anayotoa binadamu mmoja kwa mwaka. Safari zake hizo ni sawa ametumia wiki mbili akiwa angani, safari hizi ni za kibiashara na mambo yake binafsi huku akiwa hajafanya ziara ya kimuziki tangu 2017.

A-Rod

Mstaafu huyu mpira wa kikapu aliyewahi kuwa na mahusiano na Jennifer Lopez (J.LO), kazalisha tani 5,342.7 za CO2 katika safari zake 106, inakadiriwa ametumia dakika 80 kwa kila safari tangu Januari mwaka huu.

Blake Shelton

Mwimbaji huyo wa miondoko ya Country Music katika safari zake 111 alizofanya amezaliwa tani 4,495 za CO2, safari hizi ni sawa na dakika 12,424 akiwa angani.

Steven Spielberg

Director huyu wa filamu amezaliwa tani 4,465 CO2 katika safari 61 ambapo safari ndefu zaidi alitumia dakika 47, katika safari zote ametumia dakika 12,341 sawa na siku tisa angani.

Kim Kardashian

Mwanamitindo huyu na mke wa zamani wa Kanye West, katika safari zake 47amezalisha tani 4,268.5 za CO2 sawa na mara 609.8 za hewa hiyo ambayo hutoa binadamu mmoja kwa mwaka. Safari zake ni wastani wa dakika 85.49 zinazokadiriwa kuwa na umbali wa maili 99.78, huku safari yake fupi zaidi ikichukua dakika 23 huko California.

Mark Wahlberg

Muigizaji huyu amezalisha tani 3,772.85 za CO2 katika safari zake 101 ambazo ni sawa na dakika 10,428 wastaani wa siku saba akiwa angani, na hii ni katika safari za kawaida ambazo alipaswa kutumia gari.

Oprah Winfrey

Mtangazaji huyu kwa kutumia ndege yake yenye thamani ya Dola75 milioni amezalisha tani 3,493.17 za CO2 katika safari zake 68, safari fupi zaidi aliyowahi kuifanya ilitumia dakika 14 ambayo ilizalisha tani 1 ya CO2.

Travis Scott

Rapa huyu ambaye ni mpenzi wa Kylie Jenner, amezalisha tani 3,033.3 za CO2, tangu Januari ametumia dakika 8,384 au siku 5.8 akiwa angani, huku umbali wa safari zake ukiwa ni maili 7.31 ambapo inaelezwa iwapo angetumia gari, basi katika safari hizo angekuwa anatumia dakika 10 pekee!.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live