Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiyoyajua kuhusu penzi la Juma Nature na Sinta (Part 2)

Sinta Naturee Usiyoyajua kuhusu penzi la Juma Nature na Sinta (Part 2)

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Video ya Cool James Dandu, ambayo Sinta alitakiwa kushiriki kama video Queen, Location ilikuwa Mwanza, cha ajabu Video imetoka msichana bado yuko beach za Mwanza, hapa ndipo Kiroboto alipoanza kuumua wivu, ghafla penzi la wawili hao likaingia vuguvugu, moja kati ya mambo mazito yaliyokuwa yanatajwa kwenye harakati za vuguvugu hilo, ilikuwa tetesi za usaliti wa Sinta.

Maneno yaliibuka kuwa mwanadada Sinta anamsaliti Juma Nature kwa kuwa na mahusiano na wasanii kadhaa wakubwa wakati huo, akiwemo Cool James Dandu, Msanii ambaye alikuwa na heshima kubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva, Cool James Dandu ni mwenyeji wa Mwanza.

Oya madogo wa miaka ya 2000, naomba niwaambie kitu kuhusu Cool James Dandu, ambaye kwa sasa ni Marehemu, huyu ndiye muasisi wa tuzo za muziki nchini, hizi tuzo za Kili Music Awards, awali zilikuwa zikiitwa tuzo za Dandu, baada ya kufariki, ndipo kampuni ya Bia ya Kilimanjaro wakaendeleza kile alichokianzisha Dandu.

Naomba mjue ninapomuongelea Cool James Dandu, namuongelea mtu ambaye alikuwa na heshima kubwa sana kwenye Muziki wa Bongo Fleva, wakati tuhuma hizi za usaliti wa Sinta kwa Nature.

Msichana huyo alikuwa akisoma Chuo cha Uandishi wa Habari cha DSJ jijini Dar es Salaam, baadaye alipata kazi ya kuwa mtangazaji wa Clouds FM jijini Mwanza, huko nako skendo za usaliti zikamfuata na magazeti yakachombeza kwelikweli eti anatembea na matajiri wa wauza samaki.

Hatimaye, kama waswahili wasemavyo, ‘ngoma ivumayo sana hupasuka’. Penzi la wawili hao ambalo liliunganishwa na Swebe, ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa Nature, likavunjika na kishindo cha mvunjiko wake kilikuwa ni zaidi ya ulivyowahi kusikia ‘Diamond na Wema wapigana chini’.

Hii ya Juma Nature na Sinta, ilikuwa kali kwa sababu utamu wake ulikuwa wa masimulizi tu, ni kama kusikiliza mechi ya Simba na Yanga kwenye redio, unaweza kudhani ni Barcelona na Real Madrid ndiyo wanacheza. Waswahili husema maneno huumba pepo katikati ya dunia.

Baada ya kipindi kifupi, Juma Nature akathibitisha kupitia magazeti ya udaku kweli kaachana na Sinta, akaongeza kusema kuwa ataachia albamu yake mpya aliyoibatiza jina la ‘Ugali’.

Akazidi kutiririka kuwa atasimulia yote kwenye albam hiyo. Kila mwenye pumzi na apendaye Bongo Fleva alipata ‘shauku’, watu wakasubiri kwa hamu ugali ili wajue mbivu na mbichi.

Wanaume wakaendelea kushinda jikoni wakipika ‘Ugali’. Wapishi wakuu ni P-Funk Majani na Juma Nature, jiko lilikuwa Studio za Bongo Records.

Mara ikatangazwa rasmi kuwa ‘Ugali’ umeiva, na kwamba utapakuliwa kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Ukumbi ambao hata wasanii wa kimataifa walikuwa wanasita kufanyia maonesho yao kutokana na kuogopa kupwaya.

Nature Kama alivyoahidi kuongea kila kitu kuhusu uhusiano wake na Sinta, kupitia Albamu ya Ugali, ndvyo alivyofanya, nyimbo zilizokuwa kwenye albam hiyo, tatu zilikuwa zinahusu sakata hilo.

1.Inaniuma Sana

2.Staki Demu

3.Sitaki Demu Remix. Nyimbo hizi zote aliliongelea penzi lake na Sinta, Nyimbo nyingine kwenye albam hiyo ni

4. Salio la Vesi

5. Aaah Wapi

6. Umoja wa Tanzania

7. Ugali.

Katika albam hiyo, ‘Inaniuma Sana’ ambao uliokuwa mrefu, ulizungumzia kwa kina uhusiano wao tangu walipokutana na hata kusalitiana. Juma Nature aliimba kwa maumivu na uwasilishaji wake ulifanikiwa. Sana, ikawateka watu wakamuamini yeye, bila hata kusikiliza upande wa Sinta.

Baadhi ya mistari ya kwenye wimbo wa, "Inaniuma sana" Nature anasema,

Siku ya kwanza kukutana naye alikuja kwetu usiku,

Alinikuta nimechoka nimetoka ku record usiku,

Walikua kama wanne hivi ndani ya gari aina ya chaser,

Wamejaa hangover utazani jana yake walikesha,

Akaja mshikaji wangu mmoja, kutoka kwenye lilelile gari akaja moja kwa moja, mpaka kwenye mlango wa gheto

Nature nature kuna mtu anakuhitaji, embu toka umuone...

Mshikaji ambaye Nature amemzungumzia ni Swebe, kwa ambao hawamjui Swebe naomba niwaambie kuwa, huyu ni Mwana maigizo, na alikuwa kundi la Kaole Sanaa Group pamoja na Sinta.

Kundi ambalo limewatoa mastaa kibao wanaotamba sasa kwenye tamthilia na filamu, akiwemo Swebe na Mshikaji wake Beni, Steven Kanumba kwa sasa ni Marehemu, Vincent Kigosi Ray, Dkt Cheni, Mzee Magari, Muhogo Mchungu, Kingwendu, Bambo, Zembwela, Max kwa sasa ni Marehemu, Tino, Sajuki kwa sasa ni Marehemu, na wengine wengi tu ambao wanatamba kwenye ulingo wa filamu na tamthilia kwa sasa.

Hao niliowataja ni kwa upande wa Wanaume, kwa upande wa Wanawake ambao waling'aa sana enzi hizo kwenye tamthilia wakiwa na Kaole Sanaa Group, ni Sinta na shoga yake enzi hizo aitwae Nina, pamoja na Nora, huyu alitesa sana kipindi chake na mganga wake Ng'wizukulu Jilala...R.I.P.

Naweza kusema Nora na Nina pamoja na Sinta enzi hizo ndiyo walikuwa masista duu wa ukweli mjini, wakiongozwa na Amina Chifupa na Maimartha Jesse, ambao walikuwa ni watangazaji, hawa wadada ni wazuri mpaka kesho, hawana mpinzani.

Johari, Mainda, Bi Star, Bi Kidide, Nyamayao, Lulu, Dida wa kipindi cha Mashamushamu, wote hawa ni zao la Kaole, madogo wa miaka ya 2000, leo nawaambia kuwa kabla ya kuwa mtangazaji wa maredioni, Dida alikuwa muigizaji, waambieni ITV warudie Tamthilia za miaka ya 2000, muone kaka zenu tulivyopata burudani.

Kulikuwa na kundi la Kidedeaa, Mambo hayo, na Kaole, na mengineyo, nitakuja na Makala ndefu ya kuhusu Maigizo ya zamani, ngoja tumalizane na Nature na Sinta,

Nature anaendelea kumwaga mtama kwenye kuku wengi, kupitia wimbo wa Inaniuma sana.

Anasema....

Kutoka nje namkuta msichana namfahamu kwa jina la Tina,

Ambaye alisoma DSJ chuo kile kikuu cha habari na katika kipindi hichi chote alikua anaishi hosteli, mshikaji akamuita,

Akasema huyo Juma huyu hapa, sasa ongea nae muelewane, mwende mkajichane

Christina Magogi ndiyo huyo Tina, na ndiyo Sinta Kisanii,

Nature anaendelea...

Mamboo,

Safi tu. Aunt sijui unamatatizo gani?

Akang'ata vidole ili nimuone bonge la shori,

Sikujua alichotaka ila niliona ni miujiza

Mtoto mdogo wa kike kunifuata usiku ulio jaa giza

Kuanzia juu mpaka chini shepu yake ni ya kuigiza

Aunt si ushaniona mi naondoka naenda zangu kulala

Na istoshe usiku sahizi dingi akisikia ni msala

Akang'ata vidole akageukiana na wenzake alafu wakapeana Ishara

hahaha!

Kama kuna mademu kama hawa asilimia tisini watakuwa wanaugua miwaya

Hii single hailizwi hivi hivi nikikumbuka kipigo ambacho anapigwa mwizi kinacho fuatia ni kifo hata kama awe ana hirizi.

Tunarudia topic yetu samahani washikaji kwa usumbufu kwa kusikiliza maneno matamu na yenye ubunifuuu akarudi msichana akiwa na huzuni tokea jana

naomba kampani yako twende tukatese Billcanas,

ok hamna shaka twende tukafanye unachotaka,

Hapo Nature amenitupiga za uso, kusema hakujua kilichomleta Sinta usiku nyumbani kwao, ukweli ni kwamba Sinta alikuwa anatoka location, ndio maana Nature anasema Sinta alikuwa katika muonekano wa kuigiza.

Swebe ambaye ndiye aliyebuni jina la TMK Family, na kuwapa wakina Nature walitumie katika kundi lao la Wanaume, alimteka Sinta kimaneno wapitie kwa Nature kwanza kabla ya kwenda nyumbani kwao.

Sema Nature kuna baadhi ya mistari ya kwenye iliniuma sana alitupiga za uso, Kiroboto alijitetea yeye na kutaka Wabongo tuamini mrembo Sinta alimshobokea, na wakati ukweli ni yeye Nature alimpenda Sinta, mrembo ambaye kwa wakati ule, hakuna Mwanaume aliyeumbwa na kukamilika asingependa kulala naye kitanda kimoja, Sinta alikuwa ni mrembo sana, hata Nature mwenyewe alikiri hili, pale aliposema, kwenye inaniuma sana,

Nikuulizaa "Bwana weee wanawivu hao"

Wewe binadamu gani uchukiwe na kila mtu bwanaaa

Au kwakua mrembo mfupi na mzuri sanaaa

Na hao ni baadhi tu ya wale ambao nawafahamu mimiiii

Wengine ni rafiki zangu nikiwataja huwezi kuaminiii

Haya wewe si msanii nenda kalipize kwenye TV,

Watu tulimuamini Nature kwa sababu yeye ni Mwanamuziki, alitumia kipaji chake kuelezea penzi lake, tofauti na Sinta ambaye alikuwa ni mtu wa Maigizo, Kaole wasingekubali kwa kipindi kile waache kurusha Igizo la Tufani, wadili na Penzi lililokufa la Nature na Sinta, na ndiyo maana mrembo Sinta akaamua kukaa kimya tu, licha ya kuambiwa na Nature akalipize kwenye TV.....

Itaendelea......

Chanzo: www.tanzaniaweb.live