Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiyoyajua kuhusu penzi la Juma Nature na Sinta (Part 1)

Sinta Naturee Usiyoyajua kuhusu penzi la Juma Nature na Sinta (J Lo wa Bongo)

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nani anakumbuka penzi la supastaa wa Bongo Fleva enzi hizo Juma Nature na mrembo Sinta mwaka 2003? Ni mapenzi yaliyotikisa nchi katika zama ambazo hakukuwa na Facebook, WhatsApp wala Instagram.

Habari za mastaa tulizipata kwenye magazeti ya udaku tu. Juma Nature alikuwa staa mkubwa sana wa Bongo Flava na Sinta alikuwa staa mkubwa sana wa Bongo Movie.

Tasnia hizi mbili ndizo zilizokuwa zikiwindwa na magazeti ya udaku. Ni Mfalme Juma Kassim Nature kutoka Temeke, alikuwa moja kati ya wasanii wenye kuongoza kushirikishwa na wasanii wenye majina makubwa kama yeye kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Albam yake ya kwanza, ‘Nini Chanzo’ pamoja na vibwagizo vikali kwenye nyimbo za wasanii wengine alizoshirikishwa zilikuwa chanzo cha kumng'alisha Nature, hatimaye kuvishwa taji la Mfalme wa Temeke wakati huo, aliitikisa Bongo baada ya kuanza uhusiano wa kimapenzi na Malkia wa tasnia ya maigizo wakati huo, ‘Sinta’.

Uhusiano huo ulikolezwa umaarufu kupitia masimulizi mengi yaliyokuwa yanaanikwa kwenye magazeti pendwa aka magazeti ya udaku. Kila uchwao, ilikuwa ni habari ya Juma Nature na Sinta ndizo zinazouza zaidi magazeti hayo.

Kwa wale ambao mmezaliwa miaka ya 2000, niwajuze Juma Nature na Sinta ndio ‘couple’ maarufu iliyowahi kutikisa zaidi kama ilivyowahi kuwa kwa Wema Sepetu na Kanumba au Wema Sepetu na Diamond.

Picha linaanza nisome taratibu, Sinta anaibukia kwenye uigizaji enzi hizo akiwa na Vincent Kigosi ukipenda muite Ray, mara ghafla Shigongo naye huyu hapa anadondoka mtaani na magazeti yake ya udaku, ni katika wakati ambao penzi la P Didy na J Lo linatamba sana pale USA.

Kibongo Bongo mwanadada Sinta nd'o alikuwa habari ya mjini, yaani hakuna gazeti lililokua halimtaji kila lichapishwapo, oya madogo wa 2000 naomba mjue, kiki hazijaanza jana, toka enzi hizo zilikuwepo, ni Sinta huyo anawaita waandishi wa habari, anataka Watanzania tujue kuwa yeye bado ni bikra, kweli waandishi wa habari wakatuhabarisha siku ya pili yake, "Jamani eenh kuleni chuma hicho."

Sinta kumbe bado bikra! Watu tukagawanyika wapo walioamini na wapo ambao hawakuamini, basi bwana. Katika mpangilio wa kiki za huyu binti akaliteka soko, na hapo ndipo akaukamata moyo wa huyu bwana Kiroboto (Juma Nature) wakati huo akihit na pini zake kali kama Kighetogheto, Jinsi Kijana nk.

Nature alikuwa gumzo Diamond na Alikiba wanasubiri, maana alikuwa anawakilisha maisha halisi ya Watanzania halisi wa uswahilini na vijijini.

Nature alikuwa kawazoea wasichana wa kwao Mbagala Kiburugwa na Wazaramo, akamvaa kikichwa kichwa mtoto wa mjini Sinta (J Lo wa Bongo) Swebe ndiye aliyeyaunganisha mahusiano haya.

Msichana chati ikazidi kupanda wenye mihela yao wakaanza mwaga dau nakumbuka kuna tajiri wa unga alikuwa Iringa Mjini ana magari ni Mchaga aliwahi mhonga Sinta Tsh milioni 2 ili alale naye usiku mmoja tu, hii hela ilikuwa inatosha kabisa kununua gari.

Enzi hizo hakukuwa na mitandao ya kijamii, hivyo masimulizi ya mdomo ndiyo yaliyotawala zaidi. Na kama unavyojua, masimulizi ya mdomo huongeza chumvi na kukoreza utamu au hata kuharibu mboga.

Nature masikini akawa anaambiwa tabia za Sinta lakini akawa haamini. Kasikilize kiitikio cha wimbo wa "Sitaki Demu";

Walimwengu walikwisha niambia kuwa demu wangu mimi hafai (hafai) Mimi nikawabishia nikaona wao ndio hawafai (fai) Hivi sasa me najuta Sitaki demu sihitaji demu Bora nitafute mchumba Sitaki demu sihitaji demu,....

Hapo Nature alikiri kuwa Walimwengu walishamwambia kuhusu Sinta, lakini Kiroboto akawa mbishi ambapo baadaye ulizaa majuto.

Kasheshe jingine hili hapa ni Cool James mtoto wa Dandu anadondoka nchini na midola kibao, kufika Bongo anaambiwa demu mkali na wa kiki ni J Lo (Sinta) haraka sana akamuomba awe video queen kwenye wimbo wake wa mpenzi.

Nature akamaindi hakutaka Sinta akashiriki kwenye hiyo video, msichana akamtuliza, tulia baby mimi ni wako peke yako, naenda kushuti tu video hakuna kingine...."

Nini kiliendelea? Fuatilia TanzaniaWeb itaendelea baadaye.....

Chanzo: www.tanzaniaweb.live