Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Usipojiangalia, mambo haya yatavunja ndoa yako!

Happy Looking Couple In Bed Usipojiangalia, mambo haya yatavunja ndoa yako!

Thu, 26 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kila kukicha napata ujumbe kutoka kwa wanandoa ambao hulalamika kuwa hawawaelewi wenza wao kwani wamebadilika lakini malalamiko mengi yanaelekezwa kwenye tabia hizi ambazo nitakueleza hapa na kama zinakuhusu, kabla ndoa yako haijapinduka unatakiwa kuzifanyia kazi.

MOJA; HUNA MUDA KWA MWENZA WAKO Wanandoa wengi au wapenzi hawana muda wa kupumzika na wapenzi wao na kubadilishana mawazo. Hii ni kutokana na maisha ya sasa yanavyoenda. Tatizo hili au tabia hii inaweza kukusababishia mwenza wako kukukosa na kuona kuwa hana muda na wewe.

MBILI; KUSEMA UONGO Hakuna anayependa kudanganywa hasa pale ambapo hapastahili lakini pia hakuna ambaye anapenda kuahidiwa kitu kisha asitimiziwe. Baadhi ya watu tulio kwenye uhusiano, tunapenda kudanganya sana, kitu ambacho unaweza kukidharau lakini mwenza wako kikamuumiza sana.

TATU; KUTOMUAMINI Kuwa na wasiwasi na mwenza wako kila wakati ni tabia mbaya ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuivunja ndoa. Jenga imani hata kama unatilia shaka jambo flani, lifanyie kazi kwa makini na usimuoneshe umpendaye kuwa una mashaka naye mara kwa mara.

NNE; KUCHUKULIA POA KILA KITU Kama mwenza wako hakulalamikii kwa jambo baya unalomfanyia au unalomnyima, ni rahisi kujisikia vibaya. Unapokuwa unajaribu kumwambia mpenzi wako kuhusu jambo ambalo amekuumiza na limeku-changanya ni vema ili uweze kukupa furaha.

TANO; KUKACHA FARAGHA Mara nyingi wapendanao, penzi hujengwa na tendo la ndoa. Sasa ikitokea wewe ni mtu ambaye una tabia ya kupenda kupuuza tendo hilo hasa anapokuhitaji mpenzi au mumeo/ mkeo, unamkatisha tamaa mwenza wako. Kumbuka kuwa mahusiano bila ya tendo yataenda pabaya.

SITA; BIZE KUSAKA PESA Kuwa na kazi kwa ajili ya kuwaendeleza kimaisha ni muhimu hasa kwa maisha ya sasa lakini linapokuja suala la mahusiano au ndoa ukiendekeza kazi wakati wote unaweza kujikuta ukivunja ndoa au uhusiano kwa ujumla.

SABA; MATUMIZI MABAYA YA PESA Pesa ni kitu muhimu sana kwa maisha ya binadamu lakini isipochukuliwa kwa umakini inaweza kuleta balaa. Usipoangalia pesa inaweza kukupa ‘stresi’, unaweza kuingia kwenye malumbano na mwenza wako sababu tu ya pesa.

Kushindwa kwako kupanga bajeti vizuri, uchumi unaweza kushuka kwenu. Kukosekana kwa utunzaji mzuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live