Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Usikubali urafiki wa mumeo na mwanamke, hakunaga hiyo!

Mke Mume Couplees Usikubali urafiki wa mumeo na mwanamke, hakunaga!

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Niwakumbushe tu wapendwa asikwambie mtu siku zote hakuna urafiki wa mwanamke na mwanaume wengi wao mwisho wao huishia kwenye mapenzi na penzi la watu hawa huwa zito sana na ni vigumu kulivunja.

Nimeongelea mada hii kwa sababu wanawake wengi hujikuta wakilia sana pale wanapogundua mwanamke aliyekuwa akimuita wifi kutokana na ukaribu wake na mpenzi wake kumbe wanashea penzi.

Ugomvi wake huwa ni mkubwa kwa mwenza wake kwani hujiona mjinga kwa sababu wakati mwingine akiwa na udhaifu wa mwenza wake hupenda kumshirikisha huyo rafiki akidhani kuwa ataongea naye na kusawazisha kumbe ndiyo analiibua kabisa.

Ufanyeje mwanaume akiwa na rafiki wa kike?

Usimchukie haraka wala kumuonesha hupendi uhusiano wake na mumeo lakini fanya kila uwezalo kumuonesha mpenzi wako kuwa hupendi urafiki wao.

Jitahidi kuhakikisha ujengi naye mazoea ya kumfanya akujue zaidi kwani wanawake hawa hupenda kujifanya anajenga urafiki na wewe kuwa makini.

Usimshirikishe shughuli yoyote ya nyumbani kwenu wewe na mumeo hasa ikiwa ni sherehe ya familia hata mume akitaka kumualika fanya uwezalo kuhakikisha ahudhurii.

Ukiona urafiki umezidi tafuta njia ya kukaa na mhusika bila mumeo kujua umueleze kuwa hupendi ukaribu wa mumeo na yeye, kwa kero hizo moja kwa moja atajiengua taratibu na kuachana na mumeo.

Ukiona anaendelea amini usiamini huyo atakuwa mke mwenzako hakikisha umpi nafasi ya kulibomoa penzi lenu kamwe.

Kwa leo naishia hapa najua mada hii itawagusa wengi kwani ni wengi ambao wamesalitiwa na wapenzi wao au waume zao kisa urafiki ambao huzaa mapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live