Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usher atunukiwa Tuzo ya Heshima

Usher Raymond Usher Raymond

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota ya Mkali wa R&B Usher Raymond inazidi kuwaka mara baada ya kutoka taarifa ya kupokea tuzo maalum ya heshima ya mafanikio ya kazi yake ya muziki “Lifetime Achievement” kupitia Tuzo za BET 2024.

Mbali na tuzo hizo, mkali huyo yupo kwenye vipengele Vinne vya tuzo hizo “Album of the Year”, “Best Collaboration” “Best Male R&B /Pop Artist” na “Video of the Year”

Utoaji wa tuzo hizo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Peacock Theatre mjini Los Angeles nchini Marekani June 30,2024. Usher ataungana na wakali wengine waliopata heshima ya tuzo hiyo kama vile Chaka Khan, Mary J. Blige, Busta Rhymes, Lionel Richie, P Diddy na wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live