Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usher: Nilitakiwa kuwa kundi moja na Jay Z, Diddy

Usher X Jigga Muimbaji Usher Raymond akiwa na Jay Z

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muimbaji Usher Raymond anasema alitakiwa awe kwenye kundi moja na mastaa wa muziki duniani kama Jay Z, P Diddy na Pharrell Williams lakini jambo hilo halikutokea.

Usher ambaye ata-performe Super Bowl Halftime show ya mwaka huu 2024 anasema kundi hilo lilikuwa linahusu muziki na mipango ya biashara.

“Najua utachukia nikisema hili . Mimi, Jay Z, Diddy na Pharrell Williams tulitakiwa tuwe kundi moja lakini halijatokea na nilitamani nilitamani litokee, sikusema ndio wala hapana”. amesema Usher

Pia amesema alitakiwa awe sehemu ya filamu maarufu ya Dream Girl ya mwaka 2006 ikiwa na mastaa kibao kama Beyonce, Jamie Foxx, Eddie Murphy na Jennifer Hudson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live