Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ushauri: Umefeli kimaisha kama bado uko single na miaka 30+

Tiktoker Woman(2) Ushauri: Umefeli kimaisha kama bado uko single na miaka 30+

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja wa umri wa makamo amejipata katika mfarakano na wanawake wenzake katika mtandao wa TikTok baada ya kuunda vido akiwazomea wanawake ambao hawana wapenzi.

Kwa mujibu wa mrembo huyo, mwanamke yeyote hafai kufikisha umri wa miaka 30 bila kuwa na ndoa yake thabiti pamoja na pesa zake.

Alisema kwamba mwanamke yeyote ambaye ana umri wa miaka 30 kwenda mbele na hana mume pamoja na utajiri basi huyo moja kwa moja anafaa kuanza kujiangalia kwa kioo na kujiona kama mtu aliyefeli vibaya sana kimaisha.

“Kama mwanamke ambaye huna mpenzi na uko katika miaka yako ya 30s, kama huna taaluma nzuri, biashara nzuri au hata kufurahia maisha mazuri ya mtoto wa kike, nisamehe kwa kusema kwamba wewe tayari umeshafeli kimaisha,” alianza.

Aliendelea kusema kwamba miaka 30 inapaswa kuwa mpango wa kustaafu kwa wanawake, alihoji walifanya nini katika miaka yao ya 20, ambayo inakusudiwa kupata kazi zao na umakini.

“Ulikuwa unafanya nini katika miaka yako ya 20s? miaka hiyo ilifaa kuwa yako kujijenga mwenyewe. Mbona hukuwekeza kwako mwenyewe, kwa biashara yako, kwa taaluma yako? Katika miaka ya 30s hii inafaa kuwa umri wa kujipanga kustaafu kwa mwanamke. Ni wakati wa kustaafu kutoka kwa mitaa na kujikita katika kitu ambacho unataka kufanya,” aliongeza.

Katika video hiyo, alihitimisha kuwa mwanamke yeyote ambaye bado hajapata njia yake anaweza kuelekea kwenye unyogovu na hata kuathirika kisaikolojia.

“Kama hukujipanga katika umri huu basi moja kwa moja unaelekea katika msongo wa mawazo, kwa sababu fikiria hili, kama uko 30 na hauna mtu, basi unafaa kuwa tajiri,” aliongeza.

“Ukiwa na miaka 30 bila mume, wanawake wenzako marafiki walioolewa wanaanza kukuona kama tishio, kwa sababu watakuona kama unataka kuwachukulia wanaume wao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live