Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upendo wampa kicheko Marioo

Mariooo.jpeg Marioo

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Marioo baada ya mapokezi mazuri ya albam yake mpya iliyokwenda kwa jina la ‘The Kid You Know’ ambayo ilizinduliwa na nyomi ya mastaa wa Bongo movi na muziki amesema ametambua upendo mkubwa kutoka kwa wasanii wenzake.

Akizungumza , Marioo alisema ameuanza mwaka huu kwa furaha kubwa na mafanikio kutokana na ushirikiano mkubwa alioupata kuanzia kwa wasanii wenzake hadi kwa mashabiki wa kazi zake kwa namna walivyompokea.

“Nimeumaliza mwaka na kuingia mwaka mwingine kwa baraka kubwa kutoka kwa viongozi wa Serikali, wasanii wakubwa walionitangulia kwenye tasnia ya muziki ninaoufanya ikiwa ni pamoja na waigizaji ambao walijitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa albamu yangu;

“Sina kitu cha kuwalipa ila wamenionyesha umuhimu wa kukaa na kufanya kazi vizuri na wasanii bila kujali ni kina nani amefurahishwa na ukubwa wa tukio lake hakutarajia anatamani kuona umoja huo unaendelea kwa kila msanii ili kufikishana mbali kwenye sanaa hiyo.”

Marioo alisema mwaka huu umekuwa na baraka kwake kutokana na namna alivyouaga mwaka uliopita ambao amekiri kuwa ulikuwa ni wa changamoto na mapambano kutokana na sanaa hiyo kuwafanya wasanii wengi kutoa albam tofauti na miaka mingine

Chanzo: Mwanaspoti