Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unajua Marijani, Maneti, Bitchuka walicheza soka?

Bitchuka Mkl Hassan Bitchuka.

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi usingekuwa na kazi unayoifanya sasa, ungefanya shughuli gani? Hili ni swali linaloulizwa sana au ambalo wewe mwenyewe unajiuliza. Mfano daktari anajiuliza kama asingekuwa hivyo angefanya kazi gani?

Wengine wanaweza kuonekana na kipaji fulani, lakini baadaye akaangukia kwenye kipaji kingine kabisa na kukiacha kile cha mwanzo hadi watu wakashangaa.

Leo nakuletea mfano wa wanamuziki watatu wakubwa tu nchini ambao walikuwa wanamuziki maarufu sana, lakini kabla ya kuwa hivyo walikuwa wacheza soka wazuri kiasi kwamba awali walitabiriwa kuwa wanaweza kuchezea hata klabu kubwa nchini za Simba na Yanga.

Nikisema hivyo nina maana halisi kuwa walicheza kwa kiwango cha juu sana. Hao ni Marijani Rajab, Hemed Maneti na Hassan Bitchuka. Leo sitaki kuwaeleza sana kuhusu kazi zao za muziki, ila yale ambayo wengi hawayafahamu.

Marijani, aliyezaliwa Machi 23, 1955 na kufariki mwaka 1995, aliondokea kuwa mwanamuziki mkubwa nchini ambaye hata watoto wanaokuwa leo wanakuja kukuta jina lake 'likiimbwa', pamoja na nyimbo zake kama 'Georgina', 'Siwema', 'Zuwena,' 'Hanifa', na nyingine nyingi.

Kifupi ni kwamba Marijani alikuwa mwanamuziki wa bendi ya STC, Safari Trippers na Dar International. Alizaliwa Dar es Salaam maeneo ya Kariakoo. Alikuwa mtoto wa mjini haswa.

Mbali wakati anaanza muziki, alikuwa pia ni golikipa mzuri mno. Alizidakia timu mbalimbali Karikaoo na Ilala, ikiwemo timu maarufu ya Kahe FC. Kuna wakati alikuwa akitoka kucheza mpira, anaoga na kwenda dansini. Alishaanza pia kudakia timu ya vijana wa Simba. Kutokana na mahaba yake na klabu ya hiyo, wengi walitarajia kuwa angekuja kuwa kipa wa klabu ya Simba. Hata hivyo kwa kauli yake mwenyewe akiwa hai ni kwamba, sauti ya muziki, iliizidi ya soka, akawa mwanamuziki.

Mwingine ni Hemed Maneti. Mwanamuziki mwimbaji wa bendi za Cuban Marimba, TP Limpopo za Morogoro, na Vijana Jazz. Alifariki Mei 31, 1990 kwenye Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.

Mbali na kuimba na kutunga nyingi nyingi, Maneti aliyezaliwa Muheza Tanga, alikuwa pia mcheza soka mahiri.

Huenda kama asingekuwa mwanamuziki angekuwa mchezaji mzuri kama ambavyo angekuwa Marijani.

Historia inasema kuwa aliwahi kucheza timu moja ya Omari Gumbo ambaye baadaye alikuwa winga hatari wa klabu ya Simba, lakini pia akaiongoza klabu hiyo ya Msimbazi.

Lakini waliachana, Gumbo akaendea na mpira, Maneti kwa kuwa alikuwa pia na kipaji ya muziki, akaendelea nacho. Haijajulikana Maneti alikuwa shabiki wa timu gani.

Mtoto wake aitwaye Maneti Hemed alichukua kipaji cha soka cha baba yake na kuchezea klabu mbalimbali, Dar es Salaam, ingawa hakubahatika kuchezea klabu kubwa.

Mwingine ni Bitchuka. Huyu kwa bahati nzuri yupo hadi leo. Pamoja na kuwa mwimbaji mwenye sauti nyororo, akizipigia bendi karibuni zote kubwa nchini, Msondo Ngoma Music Band, na Mlimani Park Orchestrta, historia yake inaonyesha kuwa alitoka Kigoma alikozaliwa kwenda Arusha kwa masuala ya soka, ingawa pia alikuwa anajua muziki, akitega kote kote.

Alikuwa winga hatari, hivyo alipata timu mjini Arusha, lakini wakati huo huo akiendelea na kipaji chake cha muziki, ndipo alipoonekana na kujiunga na bendi ya National ya huko.

Ni bendi ambayo ilimfanya NUTA Jazz 'Msondo Ngoma' kumnyakua na safari ya ustaa ikaanzia hapo. Hadi leo ni mwanachama na shabiki wa klabu ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live