Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umri wa Wema Sepetu wazua utata

Wema+pic Umri wa Wema Sepetu wazua utata

Mon, 28 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Nasra AbdallahWakati leo Septemba 28 ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mrembo Wema Sepetu, huenda siku hiyo ikawa mbaya kwake baada ya raia kumshambulia mrembo huyo kurudisha umri wake nyuma.

 

Hii imetokea leo Jumatatu Septemba 28, 2020 baada ya Wema kupitia ukurasa wake wa Instagram, kuweka picha aliyokuwa amevaa gauni jekundu na kujipongeza kwa kufikisha miaka hiyo 30.

 

Katika picha hiyo ilisindikizwa maelezo: “Miaka 30 malaika, niliahidi kusema ukweli kuhusu siku yangu. Septemba 28, 1990 nilitoka tumboni mwa mama yangu Mariam Athuman Sumbe, nina furaha kusheherekea miaka 30 ya maisha yangu, samahani nilidanganya."

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz