Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umri wa Pharel Williams washangaza wengi

Pharrell Williams Announces Launch Humanrace Skincare Line Pharel Williams

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Jana Pharrell Williams (Mwimbaji, Mwandishi na Mtayarishaji wa Muziki kutoka Us ) ametimiza Miaka 50.

Watu wengi Wameshangaa sana Kusikia Pharrell amefikisha Umri huo Maana bado anaonekana ana Sura na umbo la Ujana.

Pharrel Williams ameanza Muziki zamani sana Ila Mwaka 2006 ndio alianza kufahamika Zaidi Mara Baada ya Kutoa Album yake ya Kwanza aliyoipa Jina "In My Mind", Kwenye Album hiyo kulikuwa na "Hit Songs" Nyingi, Mfano; That Girl, In My Mind, Baby, Stay With Me, Nakadhalika.

Mwaka 2013 Jina lake lilisambaa zaidi Duniani baada ya Kutayarisha na Kushirikishwa Pamoja na Rapper 'TI' kwenye Wimbo wa Robin Thicke "Blurred Lines".

Mwaka 2013 ulikuwa Mwaka Wa mafanikio kwa Pharrell kwani alitoa Pia Wimbo ambao mpaka sasa ni Maarufu Duniani, Unaitwa "Happy", Youtube una Views Billion 1.1, Video ya "Happy" ilichukua Tuzo ya Grammy Mwaka 2014.

"Happy" ilikuwa kwenye Soundtrack Album ya Filamu ya 'Descipable Me 2' ya Mwaka 2013.

Pharrell Williams anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dollar za Kimarekani 250M.

Wewe Binafsi unafanya kitu gani ili kuhakikisha Hauzeeki Haraka?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live