Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umeme wamzuia Diamond kupafomu Wasafi Festival

Diamond Mtwara Umeme wamzuia Diamond kupafomu Wasafi Festival

Sun, 3 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa WCB, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amelazimika kusitisha shoo yake baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.

Ishu hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Septemba 3, 2023 katika Uwanja wa Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara kulipokuwa na uzinduzi rasmi wa Wasafi Festival.

Wasanii mbalimbali walipanda kwenye jukwaa na kutoa burudani ya kutosha lakini mwishoni wakati wa Diamond ulipofika ndipo hitiliafu ikatokea na Diamond akalazimika kushuka jukaani.

Imeelezwa kuwa, uongozi wa Wasafi umeahidi kutoa shoo ya bure hii leo kwenye uwanja huo kuanzia mida ya saa saba mchana hadi kumi jioni kufidia shoo hiyo iliyokatika ghafla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live