Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulipaji Mirabaha ya wasanii, wamiliki vyombo vya habari vilio

Cosota+pic COSOTA

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

amiliki wa vyombo vya habari kanda ya Nyanda za Juu Kusini wameiomba Serikali kusimamisha mchakato wa mabadiliko ya kanuni za malipo ya mirabaha kwa kazi za wasanii kutokana na hali ya uchumi na janga la ugonjwa wa Covid-19.

Pia wameiomba Serikali kuunda chombo maalumu kitakachoshughulikia ukusanyaji wa mirabaha, usuluhishi na usimamizi kati ya wasanii na vyombo vya habari, huku wakikipinga Chama cha Hakimiliki na Hakimilikishi Tanzania (Cosota) wakidai hawaridhishwi na utendaji wake kwa kutaka kudhohofisha sanaa na vyombo vya habari.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Agosti 9, 2021 katika kikao kilichohusisha wamiliki wa vyombo vya habari (Redio, Televisheni, Cable na Online Tv) ukanda huo, Cosota na Mamlaka ya Mawasiliano kanda hiyo (TCRA) kilicholenga kukusanya maoni juu ya kanuni hizo.

Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari Nyanda za Juu Kusini, Nabii Mpanji amesema kutokana na hali ya uchumi na ishu ya ugonjwa wa Covid-19 ni bora kusimamishwa kwa mchakato huo hadi hali itakapokaa sawa.

Pia amesema kiwango kilichoidhinishwa siyo rafiki kwani huenda ikatokea mgogoro au kuua wasanii chipukizi na kushauri Cosota kufanya tathmini kabla ya maamuzi hayo ili kutoumiza upande mmoja.

"Hebu jiulize redio au televisheni ndio inamtangaza msanii, iweje chombo hicho ndio tena kihusike kulipa msanii kwa muziki wake ambao yeye mwenyewe kwanza anaomba atangazwe? amehoji na kuongeza.

"Cosota mnakuja kuharibu hebu fanyeni mpango mbadala kwa sababu kumaliza hili, mwisho mtabebeshwa lawama kwa kuharibu sanaa wapo wasanii wadogo tukisema na sisi tuwatoze tozo watakapokuja redioni sijui kama wataishi" amesema Mpanji.

Naye Isaya Mmbaya kutoka Kyela FM amesema ili kuondoa usumbufu kiitishwe kikao cha pande zote, ikiwa ni wamiliki wa vyombo vya, Baraza la Sanaa nchini (Basata) Wasanii na Cosota ili kuwepo maazimio ya pamoja ili kustawisha pande zote.

"Nyie Cosota mmekuja kuweka ukuta kati ya media na wasanii badala ya kupata mawazo ya pande zote, wasanii wao wanatuhitaji sana kuwatangaza, inakuaje mtuambie tulipe? Mimi nashauri hicho kiwango cha Sh1.5 milioni kipo juu labda ishuke hadi 300,000 ila tunaomba kukutana wote kwa pamoja" amesema Mmbaya.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Cosota, Lupakisyo Mwambinga amesema maoni yote yaliyotolewa na wadau hao, yatafanyiwa kazi na kutolewa maamuzi.

"Tumewasikiliza maoni yao kwa maneno lakini kwa maandishi, tunayapeleka kuhakikisha yanafanyiwa kazi ili kuleta maazimio na kufikia malengo ya serikali" amesema Mwambinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live