Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukweli kuhusu kinyonga anavyopata watoto

Chameleon Ukweli kuhusu kinyonga anavyopata watoto

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Si jambo la ajabu kukutana na kinyonga katika maeneo yenye miti mingi, kwa sababu wanyama hawa wa kundi reptilia, hupendelea kuishi maeneo hayo kwa kuwa ndiyo sehemu kuu ya wao kufanya mawindo ya wadudu.

Maisha ya #kinyonga yamekuwa yakiibua simulizi na dhana nyingi ndani ya jamii, mojawapo ikiwa ni kwamba wakati wa kuzaa hupanda juu ya mti kujirusha chini, tumbo hupasuka na watoto kutoka huku yeye akipoteza maisha.

Si hivyo tu, wapo pia wanaoamini mnyama huyu akinasa kwenye ngozi ya binadamu, hauwezi kutoka mpaka shangazi wa mwathirika afike akiwa mtupu ndiyo anatoka.

Lakini hizo zote ni dhana tu ambazo hazina ukweli wowote, kama anavyoeleza Alphonce Nyululu, kaimu mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani mkoani #Tanga.

Nyululu amesema kwa kawaida mnyama huyu huishi kati ya miaka mitano hadi kumi na alipoulizwa juu ya dhana ya kuzaa na kufariki kama baadhi ya watu wanavyoamini kuwa hujirusha kutoka juu, anasema dhana na mitazamo hiyo si sahihi. Amesema kinyonga hupata watoto kwa njia ya kutaga mayai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live