Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa kukutoa machozi ngoma mpya ya Prof. Jay 'Siku 462"

PROF JAY STUDIO Ujumbe wa kukutoa machozi ngoma mpya ya Prof. Jay 'Siku 462"

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna unyonge umejificha ndani ya sauti yake. Sauti yake inaonekana ikijitafuta kurudi katika ubora wa siku za mwanzo. Lakini mpangiko wa vina, mtiririko wa kuchana, mdondoko juu ya kick na snea.

Bado vimebeba uhalisia wa jina lake. Ngoma ameibatiza title hii, "siku 462." Kwanini siku 462?!

Hizi ni siku ambazo hospital iligeuka uwanja wa vita. Maradhi yakamlazimisha Professor Jay apambane mkono wa mauti usiiguse roho yake. Wakati anatibiwa Figo muhimbili kisha India.

Ngoma ipo katika temple ya chini. Vinanda na piano vikiwa vimechukua sehemu kubwa. Beat ina baraka za mkono wa producer "Bin Laden." Ila huzuni inayopatikana kwenye maneno ya chorus, ni kazi ya "Water Chilambo."

Professor anaifungua verse ya kwanza kwa mashairi haya.

Kweli nimeamini duniani tunapita/ Na hakuna wa kubisha pale Mungu anapokuita/ Nilikuwa kama mfu siku chache zilizopita/ Asante sana Mungu umenipigania hii vita/

Nikuwa kwenye ziara tunaita chaka kwa chaka/ Ilikuwa na neema na imejaa baraka/

Kwa ufupi verse ya kwanza amejaribu kueleza jinsi alivyoanza kuumwa ghafla akiwa kwenye shows hadi kukimbizwa hospital ya muhimbili.

Nilipofika muhimbili moja kwa moja I.C.U/ Asante sana Mungu kila wakati isee you/

Nilipumua kwa mashine hali ilikuwa mbaya/ Kila kona ya mwili niliwekewa mawaya/ Moyo wangu ulisimama madaktari walivyosema/ Waliupampu saa nzima ufanye kazi tena/

Nilikaa I.C.U kwa siku mia ishirini na saba/ I.C.U pasikie namshukuru Mungu baba/ Maana kila saa niliolazwa nao walipotea/ Nami nilijua muda wowote nitapotea/

Itakumbukwa "Jay" akiwa I.C.U "Mange Kimambi" alipost video clip za professor kwenye app yake. Huku baadhi ya media uchwara zikimzushia kifo. Lakini "Joseph Haule" ameamua kutangaza msamaha kwa wote Mange Kimambi akiwemo.

Verse ya mwisho Jay amerap maneno haya.

Nikiwa I.C.U yalisemwa mengi/ Clip zilichukuliwa picha zilitrend/ Nimeshawasamehe daima chuki haijengi/ Usimzushie mtu kifo Mungu hapendi/

Mwisho kabisa ngoma inafungwa kwa Chorus iliyobeba maneno ya kumrudishia Mungu utukufu. Water Chilambo anaimba kwa hisia kali maneno haya.

Bila mkono wako, neema yako, huruma zako, nisingekuwepo. Bila msaada wako na macho yako kunitazama, nisingekuwa hai."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live