Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa Gigy Money wazua gumzo

Wed, 22 Apr 2020 Chanzo: --

MREMBO anayefanya vyema kwenye filamu na muziki nchini, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amewashtua mashabiki zake baada ya kudai anatamani kufa bila sababu.

Gigy Money, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe huo ambao aliufuta baada ya muda mfupi akidai kukumbwa na hali ya kutotamani kula, kulala na anajichukia.

“Natamani kufa bila sababu yoyote, siwezi kula wala siwezi kulala kwa kifupi najichukia mwenyewe na nimekuwa dhaifu, yaani inauma ila inabidi uwe mkubwa kuelewa, sipo ‘interested’ na mtu yeyote yule wote wamenishinda,” alisema Gigy Money ambaye hivi karibuni aligombana na kumtimua nyumbani kwake na mpenzi wake raia wa Nigeria, Hunchy Huncho.

Chanzo: --