Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa Bahati kwa Diana waibua hisia tofauti mitandaoni

Ujumbe Wa Bahati Kwa Diana Waibua Hisia Tofauti Mitandaoni Ujumbe wa Bahati kwa Diana waibua hisia tofauti mitandaoni

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Msanii wa nyimbo za sekula nchini Kenya Kevin Bahati maarufu mtoto wa Diana ameweka posti ya mpenziwe ambayo imezua gumzo na kuibua hisia mseto miongoni mwa wanamitandao hasa katika mitandao ya Instagram na Twitter.

Katika posti hiyo, Bahati alimposti Diana akiomba ruhusa ya kumtafuna wikendi iliyopita ambapo Diana Marua pia alimjibu kuwa yeye mzima ni wake peke yake nzuri tena taratibu katika mapenzi yao.

“Naweza kukutafuna leo usiku Diana Marua?” Bahati aliuliza katika picha aliyoposti katika ukurasa wake wa Instagram.

“Mimi mzima ni wako peke yako, dzaaaaddyy...jinsi niipendayo...nzuri tena ya polepole!” Kwa upande wake alimjibu Bahati msanii Diana.

Wengi katika mitandao walionesha hisia za aina, ambapo mmoja alijibu kuwa kama ni mapenzi wacha wapendanie ndani ya nyumba bali si katika mitandao; “ Lakini si mpendanie ndani ya nyumba tu?” Mwanamitandao mmoja alizua ngumzo.

Chanzo: Radio Jambo