Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujinga wa Insta unaweza kuwa pesa

85567 Ujingapic Ujinga wa Insta unaweza kuwa pesa

Sat, 23 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wakazi wa Dar miyeyusho sana. Manyunyu kidogo tu utasikia: “Jamani hii mvua inatutaka nini lakini?” Dakika chache baadaye vibao vya nyumba za kulala wageni mitaani vinasomeka: “Vyumba vimejaa.” Hii ni kwa wote yaani totozi na wakware. Hutongozwa na mvua kuliko maneno.

Unakutana na ‘mabishoo’ au ‘masista duu’ mitaani. Katikati ya jiji au maeneo yale yenye mazingira matamu matamu wamelipuka pamba kama Justin Bieber na Card B. Utawaogopa na kuwapa uzito wa binaadamu wa daraja la kwanza, kumbe hawana lolote wanasaka maeneo ya kupigia picha za kupost Instagram.

Wapo wale wadwanzi wa kwenye ‘grupu’ za ‘wasapu’ kila siku anapost misosi na vinywaji vya bei mbaya. Totozi zinadata na kuanza kuomba ‘lokesheni’. Kumbe kachota kwenye ‘grupu’ jingine au kapigia picha tu. Watu wa Dar wanaishi maisha ‘feki’ kuliko bidhaa za Mchina. Ukiiga utakufa kindezi mno. Na wale madem wa Insta wanatumia muda mrefu kuhariri picha zao ili wapost. Ulichokiona Insta na akiwa ‘laivu’ ni makande na biriani. Asilimia 100 ya sura za Insta si halisi. Unaweza kudhani unaishi maeneo ya ajabu, kwamba mbona hukutani nao mtaani kwako? Kumbe wengi upo nao mtaa mmoja.

Hawa wa Instagram ndio wanaoendesha maisha ya wasanii wetu. Hawa wenye sura za mtandaoni na za mitaani. Ndiyo wanaoamua Diamond alete mafekeche ya kidwanzi kwa madem zake ili ‘atrendi’. Ndiyo chanzo cha Zari kufungasha virago vyake na Hamisa Mobetto kutengwa na Bi Sandra, kama chuya kwenye mchele.

Hawa wamiliki wa sura mbili za mitandaoni na mitaani ndiyo waliofanya Hamisa Mobetto aonyeshe kama familia ya Mond ilikwenda kumuona alipojifungua Dylan pale Aga Khan Hospitali. Ugomvi wao ulianzia hapa mpaka leo haujafikia tamati.

Hawa wamiliki wa mafekero ya akaunti huko Insta ndio wanaompeleka puta Zari. Yaani ratiba zake zinaendeshwa na hawa kenge wa mitandaoni. Hawafai hawa ndezi wa mitandaoni wana uwezo au nguvu ya kukupa au kukunyima tuzo wakiamua. Wana umoja kama nyuki.

Wasanii wanawaheshimu sana hawa kengepori wa mitandaoni. Hawa ndio huzusha bifu la Mondi na Kiba. Hata kama wasipozusha wana uwezo wa kulikuza sana au kuliua kabisa. Hawana maana hawa simbilisi. Maana wanafanya maisha ya wasanii yajiendee kama saa mbovu.

Maisha ya familia ya Mondi yapo mikononi mwa hizi sungura tope, yaani zinaweza kumfanya mama au dadaake Mondi afanye lolote ili mradi kuwakomoa.

Gigy Money unadhani ni mwehu kwa kiwango hicho? Mizuka ya watu wa Insta ndo inamtia ndimu anakuwa kama kawehuka. Ndivyo ilivyo hata kwa Amber Rutty na wengine sampuli hiyo. Kiki za Insta ndizo zilizowatoa akili kina Mariam Birian na kina Mwijaku.

Unadhani madanga au familia ya Wema ndo chanzo cha yeye kujikondesha? Au marafiki zake wa karibu? Hapana. Ni hawa vicheche wa Insta wanaowapeleka mbio mastaa wetu hawa mpaka hujikuta wanafanya mambo ambayo alikabidhiwa ibilisi na pepo mchafu, kuyafanya. Hawa ndo virusi wa matukio ya aibu kwa wasanii wetu.

Wema kajikondesha sana. Piga ua hata yeye anajutia. Kisa! Pengine ni kutaka kufurahisha watu wa Insta ambao pengine waliikebehi shepu yake kabla ya kujikondesha. Inawezekana hakutaka kufuata kile ambacho moyo wake unataka. Kwa jicho la kawaida utaona kama Wema hana furaha na lile umbile lake la sasa kama Paris Hilton.

Msanii wa dunia ya leo hafanyi kitu kwa utashi wake. Akivaa nguo anawaza watasemaje huko Instagram. Akitengeneza nywele na kucha anafikiria watu wa Insta. Ndivyo ilivyo hata katika kuchagua bwana au dem wa kuwa naye. Kwamba nikiwa na huyu watu wa Insta watanionaje? Hawa ndo chanzo cha Tiffa kuishi nje ya Madale.

Zari alishambuliwa mno na kupewa majina kama yote yenye kuashiria kuwa yeye ni mzee, kikongwe asiyefaa kuishi na bwana mdogo kama Dangote wa Madale. Maneno na majina ya ‘Bi. Tukinao’, kwa kiasi kikubwa yanaweza kuwa yalichangia kushusha ubora wa Zari kwenye mboni za Mondi. Hata kama atakataa, huo ndo ukweli.

Inakuaje wasanii waendeshwe na wajinga wa Insta ambao wengi hukaa utupu kwenye mageto yao Uswahilini huko baada ya kudanga usiku kucha hawana mbele wala nyuma. Wanayumba kwa ‘hangover’ kwa kukosa pesa ya supu, wananuka jasho na harufu ya mimoshi ya klabu. Wanakomenti wanachojisikia. Na wengi wao ni wivu tu.

Kila jambo lina faida na hasara. Wapo wanaogeuza ujinga wa Insta kupiga pesa. Miongoni mwao ni Mondi. Akitaka kufanya kitu kwa ajili ya kazi yake yoyote, anakusanya kijiji, anapiga tukio kisha anaacha watu wasemezane.

Mungu awape nini? Akili ya mtu ndiyo iliyotengenezea pesa. Heshimu mtu mwenye akili kwanza.

Ndo dawa ya watu ‘feki’ wa mitandaoni. Kuwaandalia matukio feki ili kupiga pesa zao. Lakini kuna wasanii wa kitambo wana majina wameishia kuwa watumwa wa watu wa Insta. Wanafanya wanachotaka wale wajinga badala ya wao kufanya chao. Hii dhambi haiwezi kuwaacha watu waliokuwa wanawasimamia mastaa na kuwaacha wawe kama mnara wa askari ambao kila mtu anaujua ukiwa palepale wakiupita kila siku. Mobetto kapiga pesa nyingi za hawa wajinga wa Insta kwa sababu hakutaka kufanya kile wao wanachotaka. Akataka wafuate kile anachotaka yeye wakifuate. Mastaa wengi wenye majina walishindwa kufanya hiki.

Wale wajinga wa Insta wana uwezo wa kumfanya asiyejua kuimba awe mwanamuziki nyota. Na ‘Dai’ awe mwepesi mbele ya Konde Boy watakuaminisha kuwa Tanasha haolewi na Mondi. Na Gigy Money atakuwa mke wa pili wa Alikiba. Ndiyo hao hao waliowafanya watu wajue kuwa Zari ana miaka 50 na Hamisa Mobetto ana miaka 24.

Instagram ndiko waliko wale wajinga wasiojua hata jina la Waziri Mkuu. Na hawajui kama serikali yote imehamia Dodoma. Ndiko ambako wanaona ufahari na ujanja kumsuta na kumnanga mtoto mdogo kama Nillan, ndiko ambako wanaona wivu sana Bi. Sandra kujivunia utajiri wa mwanaye Nasseb. Kuna wajinga wengi sana kule.

Ukiwa na akili kubwa unaweza kutumia ujinga wao kutajirika. Yaani unabaki kuwa na ‘laiksi’ nyingi kwa mapicha yako bila faida yoyote. Insta ndiko ambako jamii ya wajinga imejaa, wale wa kuamini kuwa upuuzi wa Freemason unafanya masikini awe tajiri bila kuhangaika. Kule kuna ‘ututusa’ kama wote.

Lakini pia wajinga hao wana faida zao. Ndo hupambana kufanya Kiba awe mpinzani mkuu wa Mondi. Yaani waliamua tu kuwa Kiba ndo kiboko wa Mondi, hawataki kujali tena kama Mondi ni mfanyabiashara mkubwa wa muziki. Na mwenzake Alikiba ni mwanamuziki mkubwa tu. Hawa ndio wanaodumisha bifu la Kiba na Mondi.

Ukiachana na wasanii wenye majina walioshindwa kuyageuza pesa, staa mwingine anayegeuka kuwa pesa isiyo na thamani ni Kiba, bado hajatumia ujinga wa watu wa Insta kupiga mawe zaidi.

Wale dawa yao ni kutengeneza tukio ‘feki’ kisha unawauzia kifekifeki, elewa tu kuwa pesa haina utaratibu wa namna ya kupatikana kama vile misa au vikao vya Bunge, njia yoyote inaingiza pesa.

Mondi anabadili deile, anajigamba sana, ana drama nyingi. Yes muziki ndo unachotaka. Muziki siyo wa Wainjilisti na Maustaadhi, unahitaji watu wehuwehu, ndo biashara ya muziki.

Kuna Bob Marley na Fella Anikulapo Kuti, unaweza kuwafuatilia ukajua Mondi ni mlokole. Ustaarabu na muziki ni kama pesa isiyo na thamani. Lazima uwe fyatu fyatu.

Chanzo: mwananchi.co.tz