Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujauzito wangu umekimbilia kwenye mbavu-Masha Love

Masha Love Mimba Kwenye Mbavu Ujauzito wangu umekimbilia kwenye mbavu-Masha Love

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo wa mjini asiyeishiwa vituko mjini, Masha Love ametoa kali nyingine kwa kudai ujauzito wake umekimbilia kwenye mbavu ndio maana watu wanashindwa kuona tumbo lake lilikua.

Masha ameyasema hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiano na Diva wa Wasafi Fm ambapo alipoulizwa kuhusu ujauzito huo anaodai ni wa muigizaji Jimmy Mafufu, ndipo alipojibu inshu hiyo.

"Unajua Diva wewe ni mwanamke kama unavyojua haya mashaka ya mimba kuna wengine zinakimbilia kwenye maziwa wengine kwenye mbavu hivyo watu wasubiri tu wataona nikijifungua," alisema Masha.

Masha alimaliza kwa kusema, yeye kwa sasa hawako sawa na baba kijacho wake na aliyempa nafasi kwa sasa katika mahusiano ni aliyekuwa x wake, Dr Kumbuka ambaye naye huwa anamkwaza lakini hana jinsi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live