Ubatizo wa Juma; si kama wa Yohana ambaye Biblia ya Kiingereza ilimwita John The Baptist. Quran ikasema ndiye Yahya.
Ubatizo wa Juma; ni wa kubariki mafanikio ya kimuziki. Sauti ya Juma ilichongea watu barabara.
Dear friends and folks: ukuu wa Juma Mbatizaji sio kwenye ngoma zake tu. Hata aliowalegezea nati, ikawa rahisi kwao kukipiga ndani ya arena ya Bongo Fleva.
Once upon a time; Juma Mbatizaji aliaminika, aliheshimika na alikubalika. Sauti yake iliposikika kwenye ngoma yoyote, wimbo husika ulifaulu usaili wa kuchezwa redioni kabla haujatahiniwa.
Ni story ya zama za Ubabylon; nyimbo zilitupwa kapuni bila natural justice. Wimbo ambao ungeandikwa featuring Jay Moe, ulifaulu usaili kabla ya kusikilizwa.
Jay Moe a.k.a Juma Mbatizaji, angeingizaje sauti kwenye ngoma mbaya? Mwanafalsafa au MwanaFA ambaye alipolishwa yamini na Rais Samia kuwa DM wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, alijiita Hamis Mohammed Mwinjuma, mguu wake kwenye game ulibarikiwa na Juma.
FA, Mtanga mwenye lafudhi ya kushawishi msamaha wa madeni IMF, aliomba ubatizo wa Juma kuingia mjini.
Juma, aliongozana na FA hadi Mawingu kwa mjenzi huru wa Bongo Fleva, Boniluv. Utatu nadhifu wa FA, Juma na Boniluv, ikatoka zawadi “Ingekuwa Vipi” Baada ya Ingekuwa Vipi, the rest ni history. FA akawa mkuuubwa! Sauti ya Juma Mbatizaji imesheheni baraka.
Bitozi wa Kinondoni, Mnyama TID, alipojiona hafanani na Hip Hop na kuamua kuimba, ngoma yake ya kwanza aliomba ubatizo wa Juma.
Bongo Records ndio kiwanda. Jay Moe aliingiza malighafi kubariki product ya kwanza binafsi kutoka kwa TID. Majani P Funk akasimamia uzalishaji. Kitu “Zeze" kilitoka fresh!
Baada ya Zeze yenye ubatizo wa Juma, safari ya TID ikawa mwanana. Siku hizi ni Mzee Kigogo. Ni soga za heri kuhusu ukuu wa Jay Moe kwenye ukuaji wa Bongo Fleva. Ameuhudumia muziki kwa uadilifu, uaminifu, juhudi na maarifa. Hakika, ametoa wengi!
Be notified; Mei 26, 2023 (Ijumaa), Jay Moe atafanyiwa induction ceremony, Alliance Francaise, Upanga, Dar.
Atatunukiwa tuzo ya maisha yenye mafanikio kwenye muziki. Atagonga hits zake zote kwa live band. 2 hours on the stage. Ndimi Luqman MALOTO