Warrent Buffet bilionea wa kimarekani aliwahi kusema tofauti kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni kwamba watu waliofanikiwa wanasema hapana karibu katika kila jambo.Pia Elon Musk aliwahi kusema hatua ya kwanza ya kujua unasema hapana,ni kujua unasema nini kuhusu ndio.
Warren Buffett na Elon Musk kauli zao zinatoa somo nyeti kuhusu watu wengi ambao wanapenda kuishi maisha ya kuwaridhisha marafiki,mabosi na ndugu na jamaa kwa kukubali kila jambo wanaloambiwa.
Watu wengi wanaihisi kusema hapana ni dhambi wanahisi kusema hapana ni kuwaumiza watu wao muhimu na wataonekana hawatoi ushikiriano kwenye mambo fulani ya msingi na yasiyo ya msingi.Mtu ambaye hawezi kusema hapana yuko tayari kupoteza muda kwa ajili ya maisha ya mtu mwingine ,yuko tayari kutoonekana msaliti hata kama anaumia na kuwa kwenye hatari kuu.mara nyingi watu ambao hawawezi kusema hapana hawajali kuhusu maisha yao na wameamua kuwazawadi watu wengine.
Mwanasaikolojia Susan Newman na mwandishi wa kitabu Cha the book of NO anasema watu wengi wana wakati mgumu sana wakukataa maombi ya wengine.
Kamwe hauwezi kuwa mithili ya Warren Buffett,Elon Musk, Diamond Platinum,Mo Dewji,Bill Gate,Maulid Kitenge, Cristiano Ronaldo kama huwezi kusema HAPANA karibu katika kila jambo.
"Tumeanza maandalizi kuelekea mchezo wetu na Namungo jana, tuna baadhi ya wachezaji wana uchovu na wengine wana majeraha lakini nina imani na wachezaji waliopo benchi kwa sababu najua wanaweza kutupa matokeo chanya" Miguel Gamondi