Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugomvi wa Marioo na Abby Chams ulianzia hapa

Marioo Abby(2) Ugomvi wa Marioo na Abby Chams ulianzia hapa

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imefahamika kuwa wasanii Abby Chams na Marioo walifanya wimbo mwingine ukiacha ule wa (Nani), lakini baada ya Marioo kujitosa penzini na Paula ambaye ni adui wa Abby Chams.

Ndipo Paula alipompiga marufuku Marioo kufanya wimbo na Abby Chams, ili kulilinda penzi lake, Marioo aliuvunja wimbo huo akaamua kumshirikisha Alikiba kwenye kipande alichoimba Abby Chams na ukazaliwa wimbo wa 'Love Song'.

"Katika Msanii ambaye nilimsapoti na najutia kumsapoti ni Abby Chams na naomba afunge mdomo wake nisimsikie tena anaongea stori ya uongo kuhusu mimi nitamfanya kitu kibaya sana," amesema Marioo.

Kwenye malalamiko yake, Abby Chams amelalamika kwamba Paula na Kajala wana mpango wa Kumshusha na kumpoteza kimuziki kwasababu tu ya chuki zao binafsi juu yake ndiyo maana wanamzibia milango ya Rizki ambayo wanaona inaweza kuwa na manufaa kwake.

Kama itakumbukwa, Paula na Abby Chams walikuwa marafiki wazuri, lakini urafiki wao uliingia doa baada ya tetesi kuibuka kwamba Marioo alikuwa anamtaka Abby Chams lakini Abby alikuwa hamtaki Marioo.

Ugomvi wao ulienda mbali zaidi hadi kwenye vichwa vya mama zao ambapo Mama wa Abby alisikika akisema mwanae hana mpango wa kummegea penzi Marioo kwasababu bado ni bikra na anaendelea kuulinda ubikra wake, tofauti na Paula ambaye anaaminika kuwa siyo shida zake kumega penzi pale inapobidi.

Kitendo hicho kilimkwaza sana Kajala ambaye naye alijibu kwa kusema asimuone tena Abby Chams kwenye himaya ya Paula na Marioo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live