Jada pickent, mke wa Muigizaji Maarufu nchini Marekani, Will smith, ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa mwigizaji bora, amekuwa kwenye kurasa na vyombo vya habari na mitandao kwa siku kadhaa sasa.
Sababu kubwa ya kutawala vyombo vya habari ni tukio la sherehe za tuzo za Oscars, ambapo mchekeshaji Chris Rock alifanya mzaha wa kuchekesha kupitia utani wa nywele za mke wa Smith, Jada, kabla ya Smith kupanda jukwaani na kumchapa kibao.
Rock alikuwa amelinganisha muonekano wa nywele wa Jada Pinkett na muigizaji wa filamu ya 'GI Jane' Demi Moore, ambaye katika filamu hiyo anaonekana akiwa hana nywele kichwani.
Muigizaji huyo wa Marekani wa kike, Jada Pinkett, ambaye anafahamika kwa filamu kama 'the matrix franchise' na 'gotham', aliwahi kuzungumzia kuhusu hali ya nywele zake katika mahojiano kadhaa na akasema kwamba alilazimika kunyoa kichwa chake kutokana na tatizo kubwa la kupoteza nywele.
Jada Pinkett ana tatizo la kupoteza nywele linaloitwa "alopecia"
Jada aliweka wazi kuwa ana tatizo wakati wa mfululizo wa kipindi chake cha 'red table talk' katika mtandao wa facebook mwezi Mei 2018.
Alisema katika video hiyo, "ni vigumu sana kuzungumzia suala hilo."
"Niliulizwa kwa nini ninafunga kitambaa kichwani mwangu. Hii ni kwa sababu nywele zangu zinanyonyoka. Iliponitokea hali hii kwa mara ya kwanza, niliogopa sana. Siku moja wakati naoga nikajikuta na nywele kibao mikononi mwangu zilikuwa zimetoka kichwani mwangu. Nilijiuliza kama nakwenda kuwa kipara?"
"Ilikuwa moja ya nyakati hizo katika maisha yangu nilikuwa nikitetemeka kabisa kwa hofu. Hivyo nikaamuwa kukata nywele zangu na nawendelea kuzikata. Nywele zangu zilikuwa muhimu sana kwangu."
"Chaguo la kuwa na nywele au lakutokuwa na nywele lilikuwa maalum sana kwangu, lakini siku moja sikuwa na chaguo hilo."
Mnamo Disemba 2021, pia aliweka video kwenye akaunti yake ya instagram na akasema kwamba alikuwa akisumbuliwa na alopecia.
Alopecia ni ugonjwa gani hasa?
Kwa mujibu Mamlaka ya kitaifa ya huduma ya afya Uingereza (NHS), alopecia ni ugonjwa unaosababisha nywele kuanza kunonyoka. Wakati mwingine inasababisha athari mpaka kwenye kucha pia.
Mara nyingi rundo la nywele hunyonyoka na kuanguka mara moja au wakari mwingine huonekana kuanguka mara kadhaa. Inaweza kuanza katika umri wowote na inaweza kumtokea mtu yeyote.
Dr Sonali Chaudhary, ambaye ni mtaalam wa ngozi huko Delhi mwenye uzoefu wa miaka 11, anaelezea alopecia, "alopecia ni neno la kitaalamu kwa maana ya kupoteza nywele ambapo nywele zetu huanza polepole kuanguka. Wanaume na wanawake wanaweza kuwa na alopecia kwa njia tofauti. Pia ina hatua tofauti."
Alisema kuwa katika hali hii, mwanzoni, nywele huanza kuwa nyembamba na inapokuwa nyembamba, hutoka kwenye mizizi na kuacha kipara au bila nywele katika eneo hilo.
Dr Sonali Chaudhary alisema, "katika baadhi ya matukio, hutokea wakati kinga yako inapoanza kufanya kazi kinyume dhidi yako. Kinga ya mwili wako huanza kushambulia 'follicles' za nywele, badala ya kupambana na aina yoyote ya maambukizi. Lakini haitokea hivyo kwa kila mtu."
Aina za Alopecia
Dk. Sonali anasema kuwa kuna hatua na aina tofauti za Alopecia.
"Aina mojawapo ni alopecia totalis, ambayo nyusi zako pia zinanyonyoka na nywele zote za mwili katika alopecia universilus zinanyonyoka."
Dkt. Sonali ametaja aina zaidi ngingine inayoitwa "non-scarring alopecia ambayo huwatokea kwa wanawake, kwa sababu za maumbile.
Mbali na hili, pia kuna Alopecia Ariata ambayo ni aina ya kawaida ya kupoteza nywele.
Hii husababisha kipara.
"Wanaume wana alopecia aina ya Androgenetic, ambayo ina athiri ngozi ya vichwa vya wanaume wengi, ziko hatua tano, nywele kunyonyoka kwa mbele na kupoteza nywele kichwani karibu na utosini."
Alisema kuwa nywele nyingi mbele ya kichwa hunyonyoka kutokana na mabadiliko ya homoni zilizopo mwilini. Tiba yake ni nini?
Dkt. Sonali ameiambia BBC kuwa ukitaka kutibu, kwanza unaangalia hali ya lishe mwilini.
"Vipo vitu vingi vinavyosababisha nywele zetu kunyonyoka, kama vile upungufu wa madini chuma au B12. Pia tunapima vitu kama D3, thyroid profile, pcos ili tatizo la ndani liweze kutibiwa kwanza."
"Ikiwa hatujui chochote kutoka hapo, basi tunapima ngozi ya kichwa, tutaona ikiwa kuna maambukizi huko."
Dalili zake ni nini?
Dk. Sonali anasema kuwa watu wanapaswa kuchukua hatua wanapoanza kuona nywele zao zimeanza kunyonyoka.
Akizungumzia ugonjwa huo kwa wanaume, alisema, "angalia kama paji la uso wako linazidi kuwa kubwa na kama mistari ya nywele inarudi nyuma na ikiwa umeanza kupoteza nywele pande zote za kichwa."
"Wanawake wanapaswa kuona mbali zaidi. Je, wameanza kuona ngozi ya kichwa hata kwa mbali?"
Dk. Sonali anaelezea kwamba alopecia haina athari kubwa katika mwili wako. Unaweza kufanya kazi zote na wakati wote huna hata haja ya kupumzika. Lakini inasababisha matatizo ya akili kwa watu.
Dk. Sonali alisema, "hapa pia ninajaribu kuhakikisha kwamba wagonjwa wangu wanazungumza wenyewe kwa wenyewe ili kupunguza msongo kidogo, ni kama kikundi cha kusaidiana."
Dk. Sonali anaelezea kwamba alopecia haina athari kubwa katika mwili wako. Unaweza kufanya kazi zote na wakati wote huna hata haja ya kupumzika.
Lakini inasababisha matatizo ya akili kwa watu.
Dk. Sonali alisema, "hapa pia ninajaribu kuhakikisha kwamba wagonjwa wangu wanazungumza wenyewe kwa wenyewe ili kupunguza msongo kidogo, ni kama kikundi cha kusaidiana."