Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchunguzi washindwa kubaini chanzo kifo cha Mohbad

Polisi Hawajapata Ripoti Kifo Cha Mohbad Uchunguzi washindwa kubaini chanzo kifo cha Mohbad

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasayansi wa Uchunguzi na Patholojia kutoka Hospitali ya Taaluma ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Lagos (LASUTH), Prof. Sunday Osiyemi amesema uchunguzi uliofanyika katika maiti ya msanii Mohbad ‘Ilerioliwa Aloba’ umeshindwa kubaini chanzo cha kifo chake.

Prof. Osiyemi aliieleza mahakama inayochunguza kifo cha mwimbaji huyo wa Nigeria kuwa matokeo ya uchunguzi wa maiti ya Mohbad umeshindwa kufahamu chanzo cha kifo hicho.

Mohbad alifariki akiwa na umri wa miaka 27, Septemba 12, 2023, katika mazingira ya kutatanisha huku kifo chake yakizua utata kwenye mitandao ya kijamii.

Mchunguzi wa kifo hicho, Hakimu Adedayo Shotobi alielezwa kuwa hitimisho hilo linaweza kuchangiwa na sababu kadhaa, mojawapo ikiwa ni kwamba ilichukua muda mrefu, takribani siku 21 kabla ya kufanyika kwa uchunguzi huo ambapo mwili wa Mohbad ulikuwa umeoza.

Akitoa ufafanuzi zaidi juu ya shauri hilo, wakili wa familia ya Mohbad, Wakili Mwandamizi wa Nigeria, Wahab Shittu alisema, “Mwanapatholojia alisema mwili ulipaswa kufukuliwa ndani ya saa 12 baada ya kuzikwa ili kuepusha kuoza. Kwa hiyo mukhtasari anaousema ni kwamba sababu ya kifo haiwezi kufahamika na unaposema sababu ya kifo haiwezi kufahamika, maana yake ni tuhuma, haiko wazi, hakuna sababu maalum.”

Wakili huyo pia alisema mwanapatholojia alirejelea baadhi ya dawa alizotumiwa marehemu Mohbad kabla hajafariki jambo ambalo lingeweza kusababisha athari ambayo ilifanya iwe vigumu kubaini chanzo cha kifo.

Shittu alisema, "Pia alienda mbali zaidi na kusema kwamba inaweza kuhusishwa na athari za dawa fulani alizopewa kabla ya kufa. Hata hivyo hakusema kwamba hajui kama ni dawa hizo ndizo zilizosababisha kifo chake”.

Mchunguzi wa maiti ameahirisha shauri hilo hadi Juni 11 kwa ajili ya uchunguzi wa Mwanapatholojia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live