Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchebe abanywa ishu ya kukata mauno na boksa hadharani, sikia majibu…

UCHEBE MAUNO Uchebe abanywa ishu ya kukata mauno na boksa hadharani, sikia majibu…

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zilipendwa wa msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Uchebe amebanywa kuhusu vipande vya video vilivyosambaa mtandaoni akiwa amevalia boksa pekee na kushindwa kutoa maelezo ya kueleweka.

Uchebe alibanywa na waandishi wa habari alipokuwa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar hivi karibuni katika uzinduzi wa albamu ya Love Sound Different ya Elius Barnaba ambapo alijibu kuhusu masuala mbalimbali ilipofika jambo hilo akaanza kuchenga.

“Sikia mimi ni mtoto wa Kiislamu kama unavyoniona. Hujawahi kuniona nikiwa na matatuu au nakunywa pombe ukiniona nimefanya hayo ndio useme sasa nimeharibikiwa,” alijibu Uchebe.

Alipoambiwa kitendo cha yeye kuonekana hadharani akikata mauno akiwa na boksa anadhani hakikinzani na dini, Uchebe aliishia kurudia maneno yake na kupoteza kuongeza neno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live