Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ubunifu:: Miji mikubwa inayoelea juu ya bahari

1cc7102f41a45049 Ubunifu:: Miji mikubwa inayoelea juu ya bahari

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mataifa ya bara Ulaya yanawazia kujenga miji inayoelea majini kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya maji baharini .

Tayari watu wamekuwa wakiishi katika miji hii kwa karne nyingi huku wengine wakijishughulisha na kilimoMarekani, inatia kila jitihada kujenga makazi makubwa ya kisasa ya jamii inayoelea ndani ya maji.

Wakati teknolojia ikiendelea kukua na kubadilika kila uchao, kuna mataifa ambayo yanatafuta suluhu bora ya kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya maji baharini na hali mbaya ya hewa.

Moja ya suluhu hiyo ni kwamba mataifa ya bara Ulaya yanawazia kujenga miji inayoelea majini.

Japo yaweza kuonekana kama filamu, ni tayari watu wamekuwa wakiishi katika miji hii kwa karne nyingi huku wengine wakijishughulisha na kilimo.

1. Amsterdam

Katika mji mkuu wa Amsterdam nchini Uholanzi, unapowasili utayaona makazi yanayoelea huku watu wanaoishi humo wakipunga hewa na wengine wakiendesha baiskeli.

Ubunifu huo wa Uholanzi ni kutokana na kupanda kwa viwango vya maji ya bahari vinavyotishia taifa hilo ndogo ya bara Ulaya.

Mjini humo pia kuna zizi la kipekee la ng'ombe linaloelea.

Mradi huo ni kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga cha mchanga mwaka 2012 kilichovuruga usafiri na usambazaji wa chakula jijini New York.

Hivyo bwana mmoja kwa jina Van Wingarden na mke wake walipata wazo la kutengeneza shamba linaloelea majini ambalo BBC, inaripoti kuwa lilizinduliwa mwaka 2019.

Shamba hilo ambalo linasaidia katika kukuza mazingira, huzalisha maziwa, jibini na yogati na kuuzwa kwa wateja wanaoishi katika maeneo ya karibu kwa baiskeli na mabasi madogo ya umeme.



Visiwa vya ReedVisiwa hivi vilivyoko kwenye Ziwa Titicaca katika mpaka wa Bolivia na Peru, kuna jamii jamii zinazoelea.

Inaripotiwa kuwa zaidi ya jumla ya watu 2,000 wanaishi katika makazi ya kuelea majini Reed.

OceanicsShirika moja lenye makao yake makuu nchini Marekani, Oceanics linatia kila jitihada kujenga makazi makubwa ya kisasa ya jamii inayoelea ndani ya maji yakiwa na nyumba 10,000 kwenye eneo la heka 75.

Mkurugenzi wa Oceanics, Mark Collinschen alisema wanajenga jengo la kudumu ambalo linaweza kuhimili hali mbaya bila kutumia makaa ya mawe au gesi.

Miji kama Jakarta na Shanghai, ambayo inakabiliwa na matatizo ya kuongezeka kwa viwango vya maji ya baharini, kukumbatia mradi wa ujenzi wa miji inayoelea.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke