Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Uaminifu wamuepusha na kifungo cha Maisha

Most Prolific Speed Camera In The UK Has Caught Almost 50 000 Drivers This Year   2022 12 26T143056. Uaminifu wamuepusha na kifungo cha Maisha

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji na Mchekeshaji kutoka Marekani Tim Allen mnamo mwaka 1978 alikamatwa na madawa ya kulevya Kalamazoo/Battle Creek International Airport, Michigan, Marekani.

Baada ya kukamatwa na madawa hayo (Grams 650 za Cocaine) walimuomba ataje watu wengine wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya kisha kifungo chake kitapunguzwa.

Kwa mujibu wa sheria za mwaka huo mtu mwenye kosa la namna hii hukumu yake ni kifungo cha maisha, hivyo kama Tim Allen angekataa dili hili basi angefungwa kifungo cha maisha.

Tim Allen aliamua kutaja wahusika wa biashara ya madawa ya kulevya kisha akapelekwa jela na akaachiwa huru baada ya miaka miwili na miezi minne.

Mpaka sasa Tim Allen ana miaka 70, ana mke mmoja na watoto wawili "Katherine" na "Elizabeth". Tim Allen anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 100 za kimarekani. Amejizolea umaarufu mkubwa duniani kupitia filamu ya "Santa Clause" na "Christmas with the kranks".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live