Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

USHAURI WA DAKTARI: Kujamiiana wakati wa hedhi ni salama kiafya?

81880 Dk+Shita+Samwel USHAURI WA DAKTARI: Kujamiiana wakati wa hedhi ni salama kiafya?

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dokta Shita habari, pole na kazi. Mmi ni msichana mwenye umri wa miaka 21 kwa bahati mbaya nilijikuta nashiriki mapenzi na mpenzi wangu bila kinga nikiwa katika (hedhi), je kuna madhara? Na ninaweza kupata mimba?

Hili ni swali ambalo nimekua nikiulizwa mara kwa mara na wasomaji wa safu hii. Leo nitalijibu swali hili kwa kuwajuza dondoo kadhaa zitakazowapa na wengine ufahamu.

Jibu ni kuwa hakuna madhara kujamiiana wakati wa hedhi, kisayansi inakubalika kwani kufika kileleni kunapunguza maumivu wakati wa hedhi na kupunguza idadi ya siku za hedhi.

Lakini kidini, kitamaduni na kijamii kushiriki tendo katika hali hii inaelezwa kama ni uchafu na uharibu murua wa tendo hilo na hata msisimko unapungua kutokana na hali hiyo kuonekana inawaathiri wenza kisaikolojia.

Kitendo cha kuona mashuka yanachafuka kwa damu hiyo hakiwezi kuwafanya wenza kutamani tendo hilo na pia huwafanya kupata woga ambao moja kwa moja huondoa hamu ya kujamiiana.

Tendo hili wakati wa hali hii huwa na athari za kiakili (hisia) kwani hofu, wasiwasi na woga kwa vijana wakiume huwa juu kipindi hicho hiyo ni kutokana hali ya kuona damu.

Pia Soma

Advertisement
Uwepo wa athari za kihisia kama vile woga hafifisha hamu ya kushiriki tendo hilo na kufikishana kileleni.

Wataalam waliotafiti maelfu ya wanawake wanaeleza kuwa kujamiiana wakati wa hedhi hakuna madhara kiafya bali zipo faida kadhaa ikiwamo kuongeza kasi ya ushukaji wa hedhi kwa haraka hivyo kuisha mapema zaidi.

Hii ni kwa sababu wakati mwanamke anapofika kileleni misuli ya nyumba ya uzazi hujikunja na hivyo tando laini (hedhi) hujinyofoa na kutiririka.

Wakati wa kujamiiana mwanamke hupata hisia nzuri kutokana na kuzalisha kwa kichochezi(hormones) kinachojulikana kama Endophins ambacho hufanya mtu kuwa na hisia chanya ikiwamo furaha.

Kwa wale wanawake wenye tatizo la kipanda uso (migraine) kinachojitokeza zaidi wakiwa kwenye hedhi hupata ahueni wakifanya tendo hilo kipindi hicho.

Pamoja na kushiriki tendo hilo kuna faida hizo lakini kunaongeza hatari ya maambukizi kirahisi ikiwamo VVU, virusi vya homa ya ini na magonjwa yanayoenea kwa kujamiiana na kugusana na damu.

Vilevile kipindi cha hedhi kwa mwanamke mwenye maambukizi ya virusi vya hepes humwambukiza mwenza kirahisi. Mwenye virusi hivyo hupata vipele vyenye maumivu katika sehemu za siri.

Hali ya kuwa katika hedhi huibua pia maswali endapo mtu anaweza kubeba mimba kipindi hicho, jibu ni kuwa uwezekano ni mdogo sana kupata.

Kama una mzunguko mfupi ikiwamo wa siku 21 au mzunguko unaobadilika badilika kila mwezi hatari ya kupata ujauzito kipindi cha hedhi huwa ni kubwa endapo utajamiiana bila kinga.

Pamoja ya kwamba ni salama kiafya nihitimishe swali hili kwa kushauri tu vizuri kuvumilia hali ya hedhi ipite na endapo itashindikana basi vyema kutumia kondomu.

Chanzo: mwananchi.co.tz