Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UREMBO: Epuka makosa haya unapojipodoa

84646 Vipodozi+pic UREMBO: Epuka makosa haya unapojipodoa

Mon, 18 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kujiremba ni asili ya wanawake kote duniani, tofauti na nchi na aina ya mapambo kulingana na tamaduni za eneo husika.

Kwa Afrika kuna utamaduni wa kupaka wanja chini ya macho na juu kwenye nyusi.

Urembo huu umekuwa ukibadilika kila mara kutokana na kuchanganywa na kile kinachofanywa kwenye nchi za Magharibi.

Wanawake wanaopenda urembo huu kutokana na maboresho yanayofanyika walikuwa wananyoa nyusi kiasi maarufu ‘kutinda nyusi’.

Baadhi yao wamekuwa wakizitinda sana, badala ya kuzisawazisha kidogo na kupaka wanja.

Kwa bahati mbaya baadhi yao huzitinda sana au kuziondoa kabisa na kujichora wanja, huku wengine wakitumia wanja wenye rangi nyeusi na kuonekana tofauti badala ya kupendeza.

Hii ni miongoni mwa makosa yanayofanyika wakati wa kujipodoa. Lengo la kujipodoa upendeze na si vinginevyo.

Unachotakiwa kufanya ni kuzipunguza zile zilizokaa nje ya mstari kidogo kwa kuziweka kwenye mpangilio.

Baada ya hapo badala ya kuzichora kwa wanja wenye rangi nyeusi, tumia wa rangi ya uzurungi (brown) kuzijaza.

Ili ujipodoe kwa raha na unadhifu zaidi tumia wanja mnene au wa kwenye mikebe ambao ni laini.

Wanja wa penseli nyembamba licha ya kutumika miaka mingi umekuwa ukichubua eneo la kwenye nyusi usipokuwa makini.

Chanzo: mwananchi.co.tz