Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Tyson Fury atarajia mtoto wake wa Nane

Tyson Fury And His Wifeee Tyson Fury atarajia mtoto wake wa Nane

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia maarufu kutoka nchini Uingereza Tyson Fury, ameweka wazi kuwa anatarajia kupata mtoto wa nane na mkewe Paris Fury.

Fury ameweka wazi suala hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuposti picha ya mkewe huku akimwagia sifa kwa kudai kuwa licha ya kuzaa naye watoto saba lakini bado mkewe huyo ni mrembo.

Hata hivyo bondia huyo wa ngumi za kulipwa amesema kuwa yeye na mkewe hawatoishia watoto hao kwani wanampango wa kuwa na familia ya watoto kumi.

Fury na Paris wamekuwa katika ndoa kwa kipindi cha miaka 15 ambapo mpaka kufikia sasa wamebahatika kupata watoto saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live