Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyla aahirisha tour yake kisa majeraha

Tyla Msa.jpeg Tyla aahirisha tour yake kisa majeraha

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi wa tuzo ya Grammy 2024 (Best African Music Performance) Tyla Laura Seethal 'Tyla' kutoka South Africa kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kuwa ameahirisha kufanya Tour yake ya muziki kutokana na majeraha yanayomsumbua kwa muda mrefu.

Tyla hajaweka wazi anasumbuliwa na majeraha gani lakini ameeleza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitafuta tiba lakini hazijamsaidia kuepukana na maumivu hayo, hivyo bado anaendelea kupambana apone na arejee kwenye kazi yake.

Tyla ameeleza kuwa atahatarisha afya yake zaidi kama atalazimisha aendelee na Tour yake.



"I've seen doctors and specialists with high hopes but the pain has only become more agonizing as has the severity of the situation,"

"In consulting with medical professionals it's become increasingly clear that continuing any festival or tour dates would jeopardize my long-term health and safety."--Tyla.

Tyla ameahirisha show ambazo ilibidi hivi karibuni afanye kwenye Bara la ulaya pamoja na Amerika Kaskazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live