African Princess kama mwenyewe anavyojiita lakini jina lake halisi ni Fausta Charles Mfinanga maarufu kama nady amefunguka kuhusu sababu ya kulitosa Tamasha la Wasafi Festival.
AKizungumzia hilo baada ya Diamond kuwakaribisha mastaa karibu wote wa Bongo akiwemo Kiba, Harmonize na nandy, mwanadada huyo amedai kuwa tamasha hilo halimhusu.
"Mimi sina shida na Wasafi, shughuli wanazofanya kwa sasa hazinihusu, ikifika muda zikanihusu tutafanya nao kazi! Kwenye interview nilikataa kuenda sababu waliniita kipindi nakuwa mzazi," amesem Nandy.
Wasafi Festival imezinduliwa rasmi wiki iliyopita na itaanza kuunguruma katika mitaa ya Nangwanda Sijaona pale Mtwara mwezi ujao huku tayari mastaa watakaopanda jukwaani katika mikoa yote 10 wameshatangazwa juzi Jumamosi.
Nini maoni yako?