Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutanunua drone tupime ardhi” Lukuvi

Screenshot 2021 11 27 At 11.30.24 660x400.png William Lukuvi

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali inatarajia kufanya mapinduzi katika sekta ya Ardhi ikiwemo kutumia ndege ndogo zisizo na rubani “Drone” kwa ajili ya upigaji picha wa maeneo nchini.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo Dar es Salaam leo kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Taasisi ya Wapima Ardhi Tanzania (IST)a

“Tunaandaa mradi mkubwa wa kupanga na kupima Nchi nzima, tutanunua vifaa vingi vya kuongeza alama ya upimaji, tutanunua na ndege kwa ajili ya upigaji wa picha Nchi nzima ili kurahisisha kazi, tunataka tununue na ndege za drone za kila mkoa ili tupime maeneo madogomadogo kwa vifaa vyetu, tunataka tufanye mapinduzi makubwa” Waziri Lukuvi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live