Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunda Man kuuza nyumba kisa Kagere

60738 Pic+tunda+man

Fri, 31 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere ametwaa tuzo mbili za 'Mo Simba Awards' Mchezaji Bora na Mfungaji Bora wa msimu uliopita akifunga mabao 23 kwenye Ligi Kuu Bara na akifunga mabao sita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Muimbaji wa muziki wa kizazi Tunda Man, alisema mshambuliaji huyo asifikilie kuondoka Simba kwani hata kama tatizo ni pesa yupo tayari kuuza nyumba yake anayoishi ili abaki Msimbazi.

Tunda alisema; "Kagere amekuwa na mchango mkubwa pengine zaidi ya vile tulivyotarajia mwanzo wa msimu, katika kuhakikisha natambua mchango wake hatupo tayari kumuacha aondoke.

"Nimejenga nyumba kwa ajili ya kazi zangu na muziki lakini kama uongozi wa Simba itatokea kipindi Kagere atataka kuondoka kipa pesa nipo tayari kuuza hiyo nyumba yangu ili kumpa pesa Kagere aendelee kubaki katika timu yetu," alisema.

"Nawaomba viongozi wa Simba kutambua na kuelewa mchango na thamani ya wachezaji kama Kagere ambao wanapambana mwanzo mwisho kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri kuendelea kuwabakisha ndani ya timu na tupo tayari kushirikiana nao ingawa sidhani kama tunaweza kufikia huko," alisema Tunda.

Tunda aliyasema maneno hayo mara baada ya kumalizika kwa sherehe za Mo Simba Awards zilizofanyika jana Alhamisi, jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz