Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunda Man: Tukifungwa na Yanga Siimbi tena

Tunda Simba Jeneza Nsd.jpeg Tunda Man

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni shabiki wa Klabu ya Simba, Tunda man amesema kuwa endapo timu yake itafungwa na watani wao wa jadi, Yanga katika mechi ya Oktoba 23, 2022 basi ataacha kuimba nyimbo za Simba.

Tunda amesema hayo kuelekea dabi ya kariakoo kati ya Simba na Yanga itakayopigwa kwenye Dimba la Mkapa, Dar es Salaam, ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ikumbukwe kuwa, katika mechi tano za misimu miwili ambazo SImba na Yanga wamekutana, Yanga ameshinda mechi tatu na kutoa sare mbili wakati Simba akiwa hajashinda mechi hata moja.

"Kwa mchezaji mmoja mmoja, sisi tunawachezaji wazuri, kwa hiyo point kubwa ilikuwa ni kocha, kila kocha anayekuja anakuwa na mfumo wake ndiyo kupata team work inakuwa ngumu.

"Lakini amekuja #Mgunda amefanya vizuri mechi mbili hizo, hivyo kuhusu suala la timu nina timu nzuri na bora na inapambana, Nina Phiri na Okrah ambao huwezi kuwapata kule Yanga. Sasa hivi nikifungwa tena na mtani siimbi tena nyimbo za Simba." amesema Tunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live