Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunapoivisha utukufu brand ya WCB ‘kindezi’

77602 Mond+pic

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara Paap. Umetoka kisanii umekuwa staa flan hivi wa muziki. Katika pita pita zako, mtoto Wolper huyu hapa. Kajiangusha kwenye 18 zako. Humuambii kitu, hasikii la muadhini wala mnadi swala kwa penzi lako. Mungu akupe nini, gunia la chawa? Lazima utazama mazima. Kwanza ni dem mkali, halafu pili ni staa mkubwa.

Huwezi kutaka kujua mambo yake ya nyuma ya pazia. Unaanzia pale ulipomkuta na kwenda mbele. Wolper pekee kwa ukubwa wa jina lake, ana ‘kuofa’ vitu vingi. Kwanza thamani yako kama msanii inapanda. Pili kazi zako za muziki zinapata mashabiki wengi. Si kutaka kujua ubora wako, bali kumsikiliza bwanaake Wolper.

Wolper kwako anakuwa ni mpenzi na nusu. Anakupa burudani ya penzi na pesa kupitia lundo la mashabiki wa kazi zako. Ana mashabiki wa nje ya jukwaa la muziki. Hata kama ndani ya mashabiki wake kuna machizi muziki. Lakini ni wale wanaowafuatilia kina Dai, Kiba na wakubwa wengine. Siyo ‘andagraundi’ ambaye ndo unatoka.

Harmonize hakuwa boya kuatamia kwa Wolper. Hata mimi si tu ningeatamia bali ningetotoa na vifaranga kabisa. Mtoto flani hivi toka mikoa ya Kaskazini. Mbishi mwenye kuijua pesa. Maisha ya kutaka kuishi na ‘madem’ Wainjilisti yalitoweka na lile Azimio la Zanzibar, 1992. Hii ilimsaidia sana Diamond. Baada ya kujiweka kwa Wema wakati anatoka. Alimpa kiburi kiasi cha kuanza kuvimba kabla hajawa staa mkubwa. Wema alikuwa mpenzi na nusu, akimfurahisha ‘Dai’ na mashabiki wake. Waliosema bwanake Wema yuleee, akipita mitaani. Walikuwa wengi kuliko waliosema Diamond yuleee.

Kwanza hakuwa mpenzi na nusu tu. Bali alikuwa mpenzi na robo tatu. Kiingereza unachosikia kwenye kinywa cha Dangote. Kwa kiasi kikubwa Mwalimu wake mkuu alikuwa Wema. Hili lilikuwa penzi lenye faida kubwa kwa Simba wa Tandale. Kuwa watoto wenye faida ndo ujanja. Hapa dogo alichanga karata vyema.

Watu tumeumbwa kusahau tu. Wema wa wakati ule, kila mtu alishangaa ‘kudeti’ na Mondi. Anampa nini? Kampendea nini? Mbona hawaendani? Kwanini anajichoresha?

Pia Soma

Advertisement
Hayo yalikuwa maneno ya wengi, ambao hawakuamini kutoka na Mondi. Mwisho likageuka kuwa penzi la mastaa maarufu zaidi.

Msela wa Tandale akawa mkubwa kwa uwepo wa Wema kando yake. Hakuwa na cha ajabu kiasi cha kujaza watu pale Mlimani City. Na kuweka historia kwenye mtiti wa show ya Diamond Are Forever. Ile ni akili kubwa ya burudani toka kwenye utosi wa Ruge Mutahaba, aliyeona fursa ya ‘drama’ za ‘Dai’ na Wema.

Harmonize kapitia njia hizo. Naye baada ya kusumbua na singo moja tu akajiweka kwa Jack Wolper. Wanoko wengi hawakuamini kama dogo amejimilikisha hili toto la Kichaga. Afadhali ya “Dai’, aliaminika haraka kutokana na tabia za Wema. Alijiweka kwa yeyote akimuelewa. Wolper hakuwa wa ‘taipu’ hizo.

Wolper aliaminika kama ‘dem’ wa matumizi anayehusudu mkwanja mrefu. Mmakonde mwenye singo moja atampa nini? Wanoko waliamini kwenye ‘drama’ zaidi ya penzi la kweli kwa wawili hawa. Wolper ni ‘levo’ za Dallas anayehonga BMW X 6 anayotumia Dai, bosi wa Harmonize. Inakuaje sasa?

Viulizo na ‘skendo’ za hapa na pale zikamkuza Harmonize. Akaanza kuvimba, siyo kwa muziki tu. Bali umiliki halali wa nyonga za mtoto wa Kichaga. Kama bosi wake, naye umaarufu ukapanda kwa kasi. Akapita kwenye reli za kaka yake kupanda chati. Mashabiki wakamuunga mkono kwa kila hatua.

Wakati wanaanza penzi lao, Wolper alikuwa na ‘bezi’ kubwa ya mashabiki kuliko Harmo. Akagawa raha na kuongeza lundo la mashabiki kwa Konde Boy. Hata walipomwagana bado Harmo akaendelea kupanda juu kwa sababu tayari alikuwa mkubwa kisanii. Na ‘Team’ WCB wakamuunga mkono.

Konde Boy kwa kiasi kikubwa ameiga kila kitu, kama pozi na swaga za Dai. Mashabiki wa WCB hawakujali. Na hata pale mashabiki wa Wolper, walipoendesha kampeni chafu baada ya kutemana. WCB hawakuacha kumuunga mkono. Na kuonyesha watu kuwa baada ya Mondi anayefuata ni Konde Boy na huwaambii kitu.

Alimuiga sauti. Kimya! Akaiga swaga na staili ya uimbaji. Kimya! Akaanza kupita njia za kaka yake kama kujimilikisha mtoto Jack Wolper. Kimya! Akafanya ‘kolabo’ na wasanii wakubwa Afrika. Kimya! Ndo kwanza akawekwa mbele ya wasanii wengine wakubwa. WCB walitaka kutuaminisha kuwa baada ya Dai ni Konde Boy.

Leo hii anaiga jambo la msingi zaidi kutoka kwa Dai. Akitaka kujitegemea na kuendesha shughuli zake kivyake. Kitu ambacho ni kina maana kubwa kwa maendeleo yake binafsi na tasnia ya muziki. Wale wale waliomsapoti kwenye udwanzi mwingi. Kwenye hili la msingi zaidi wanamkataa. Huwezi kujua wanachotaka mashabiki wa WCB. Alipoiga ujinga kama kubadili totoz walisapoti. Alipoiga kupaka rangi nywele wakamsifia. Alipofanya kazi na wasanii wakubwa Afrika aliungwa mkono. Hili la kujitegemea hawataki. Wanamuona mhaini asiye na shukurani na asiyefaa kuwepo.

Nimetumia mwezi mzima, kutafuta kosa la Harmo silioni. Zaidi naona faida kubwa kwake na kwa tasnia ya muziki. Kwanza anaacha nafasi ya wengine kujiunga WCB. Pili anaenda kuongeza ‘brand’ nyingine ya kuwatoa kisanaa kina Harmo wengine.

Watu hawataki, wanataka kuona yuko chini ya watu ‘deile’. Anaendelea kumuiga kaka yake. Kwa kuanzisha kitu kingine cha kusaidia watu wenye vipaji vya muziki. Ili awashike mkono nao watoke kama yeye alivyotolewa na Mondi. WCB wanakasirika. Wananuna na kumsemea mabaya. Hawataki uwepo wa kampuni mpya za kusaidia kina Konde Boy wengine?

Hawataki WCB wazibe nafasi ya Harmo kwa kusajili kipaji kingine kinachosota mtaani? Wanataka WCB iwe na wasanii wale wale? Hawataki wasanii wa WCB wakue na kujitegemea kivyao? Sasa waliletwa ili wafie WCB? Vigumu kuwaelewa hasa wanachotaka mashabiki wa WCB.

Waliyemsapoti kwa kila kitu. Leo wanamuombea apotee kisanii. Wanajaribu kuwapa utukufu uongozi wa WCB kama ni watu wasiokosea. Kwamba wanaotoka WCB kwenda kutafuta kwingine watakumbwa na laana ya kupotea kisanaa. Kosa la Harmo ni kuondoka WCB tu? Diamond hakuanza na WCB miaka 10 iliyopita. Alipita kwenye mikono ya watu wengi na kuachana nao. Hali hiyo ndiyo iliyompaisha hii leo yumo pale alipo. Angeendelea kuwa chini ya Papaa Misifa? Alipoachana na Papaa Misifa mtu aliyemtoa kisanii, nani alimlaani Diamond? Papaa Misifa aliachana na Mondi kibwege. Pamoja na yeye kumuamini kwa kuweka pesa kwa ‘Dai’ akiwa si chochote, lakini Mondi hakuondoka kiungwana alipofanikiwa. Pia alitemana na Ruge ili afanye shughuli zake kama mtu huru. Mbona hatukusikia akilaaniwa na watu.

Kama kutemana na hao watu kulimsaidia Mondi afike pale alipo, kwa nini kwa Konde Boy kutemana na ‘Dai’ ionekane atakufa kisanii? Au tumeamua kuwavisha utukufu WCB? Dogo kishafunguliwa milango, anataka kusimama kivyake, watu wanatoa maneno ya kumlaani afeli. Ili?

Kwa tabia za WCB, Harmonize angeondoka kwa ubaya tungesikia. Ndo maana kuna hisia kwamba WCB, huenda wanatengeneza ushindani wa Dai na Konde. Ili kufuta taswira ya upinzani wa Mondi na King Kiba. Hisia hizi zinakuja kutokana na imani kuwa Harmonize hawezi kuondoka WCB kibwege tu.

Na mpaka sasa tayari kila sehemu ni Konde Boy na Mondi. King Kiba pamoja na sakata la ndoa yake, lakini akili na masikio ya wadaku yako kwa WCB na Konde Gang. Kama lengo ni kufuta upinzani wa Mondi na Kiba, kwa kiasi fulani kuna harufu ya kufanikiwa. Ingawa haina maana kwa uhai wa tasnia ya muziki.

Udwanzi si kuondoka WCB. Ila kubaki WCB wakati uwezo unao, huo ndo udwanzi mbatata. Pisha watu wengine wajiunge WCB wewe ukienda kutengeneza WCB yako, ambayo itatanua wigo wa ‘brand’ za kutoa wanamuziki wengine. Team WCB waache kumuwaza Konde Boy. Kuna Makonde Boy kibao mitaani.

Chanzo: mwananchi.co.tz