Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuko duniani muda mfupi, tuinjoi maisha-Zari

Zari One Tuko duniani muda mfupi, tuinjoi maisha-Zari

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zari The Boss Lady amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kuonekana na kijana mmoja ambaye ni mdogo mno kiumri akimtambulisha kama mumewe.

Zari amezungumziwa sana baada ya picha na video zake za mahaba na kijana huyo kusambaa na ilimbidi ajitokeze na kumtetea kijana huyo kwa kuweka wazi kwamba cha muhimu kwa sasa ni mapenzi yake na kijana wa watu na wala si maneno ya watu.

Zari anasema kwamba katika maisha haya hatupo hapa duniani kuishi kwa muda mrefu na kuwataka watu wafanye bidii na jitihada katika maisha kisha kujiliwaza kwa kujitunza vizuri kwani duniani tupo kwa ajili ya muda na nyakati nzuri na wala si kwa muda mrefu.

“Ikiwa unafanya kazi kwa bidii, jivinjari kwa tafrija nzuri mwenyewe. Tuko hapa kwa wakati mzuri na siyo muda mrefu,” anasema Zari.

Wengi walitafsiri ujumbe huo kwamba alimaanisha kujivinjari ni chaguo la mtu na kitu chochote anachokiona kinastahili kumpa tafrija ya moyo wake hivyo ni kama njia moja ya kuwasuta wale wanaomuwekea vikwazo na viwango vya watu anaofaa kuchumbiana nao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live