Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuerny afunguka madai ya kuwa na uhusiano na Diamond

Tuerny Na Diamond Tuerny afunguka madai ya kuwa na uhusiano na Diamond

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo maarufu mitandaoni Tuerny amefunguka kuwa yeye na Diamond ni watu wenye uhusiano wa kawaida.

Akijibu swali la kuhusishwa kuwa na uhusiano na Diamond kwenye kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, Tuerny alianza kueleza sababu za yeye kufuta picha zote kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumposti Diamond.

“Nilifuta picha kwa ajili ya kuanza upya kwenye ukurasa wangu wa Instagram. Nilimposti Diamond kwa sababu picha ile ni kali kuliko zote.

“Diamond hatuna ushkaji hivyo sema ni mtu ambaye ninahudhuria tu mambo yake mengi anayotualika. Nimemposti kwa sababu tu nimejisikia na si vinginevyo,” alisema Tuerny.

Mrembo huyo kwa sasa amejiingiza kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live