Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuachane na mambo ya Kagoma, tu-focus na mechi yetu - Manara

Manara Kamwe Mdz Tuachane na ya Kagoma, tu-focus na mechi yetu

Sat, 14 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaandika Haji Manara;

Na mimi nalisoma na kulisikia Sakata la mchezaji Yussuf Kagoma kama tunavyosikia wengi... Ningeshauri jambo kwa Wanayanga wenzangu, hebu tufocus na mechi ngumu ya kesho ugenini dhidi ya Wahabesh.

Wachezaji wetu wanasoma mitandaoni mabishano yetu na Watani zetu, na wao kama binadaamu wanaingia katika mkumbo wa kipi iko focus zaidi. Tuitumie siku ya leo na kesho kuwaombea Mungu wafanye vizuri,tuwaonyeshe hili la kesho ni muhimu zaidi kwetu kuliko kuhangaika na jambo ambalo TFF bado hawajafanya maamuzi!!

Let’s focus na vitu serious zaidi, hilo lingine tuliweke kiporo kwanza, tuwaambie Wachezaji wetu tunahitaji kufuzu Group Stage kuliko kitu chochote kile kwa hivi sasa, tuwape nguvu na tuwaonyeshe kwamba tunawaamini na tunawategemea wao pale Addis Ababa hiyo kesho.

Hamasa yetu huku na mitaani wanaisikia na kuiona, na always huwapa nguvu kubwa ya kupambana zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live