Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trey Songz azimia kwenye kesi yake

Trey Songz Trey Songz azimia kwenye kesi yake

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia iliyokuwa ikimkabili staa mwimbaji wa Marekani Trey Songz hatimaye imefikia ukomo baada ya mtuhumiwa kukubali kulipa Dola Mil.25 sawa na Tsh. Bilioni 64.4 nje ya mahakama.

Habari za ndani zimefichua hivi majuzi katika nyaraka za kisheria ambazo gazeti la The Blast limezipata, zikionyesha kuwa mwimbaji wa "Say Aah" na mlalamikaji, Jane Doe, wamemaliza tofauti zao nje ya chumba cha mahakama.

Ikiwa masharti ya kusuluhisha yametimizwa, ombi la kufutilia mbali kesi hiyo linaweza kuwasilishwa kabla ya Juni 10, 2024.

Kesi ya mwimbaji huyo ilianza mwaka 2022 wakati mwanadada Jane Doe alipomshutumu kwa kumnyanyasa kingono kwenye moja ya party aliyoalikwa nyumbani kwa Trey Songz mnamo Agosti 2015.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live