Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Trela ya Reality Show ya "The Kardashians" yawashtua Mashabiki

Kardashians Trela ya Reality Show ya "The Kardashians" yawashtua Mashabiki

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Trela inayoendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ya reality show ya familia maarufu nchini Marekani ‘The Kardashians’ imewashitua mashabiki baada ya Krish Jenner kudai kuwa ana tatizo la kiafya.

Kupitia trela hiyo Krish Jenner amewafahamisha binti zake kuwa miezi kadhaa iliyopita alikutana na daktari wake ambaye aligundua kuwa ana uvimbe mdogo ambapo haijawekwa wazi ni uvimbe wa nini.

Aidha kufuatia na taarifa hiyo iliwashitua watoto wake Khloe Kardashian, Kylie Jenner, na Kendall Jenner, huku baadhi yao wakitoka na machozi. The Kardashians on Hulu’ inatarajiwa kuanza kuoneshwa tena Mei 23 mwaka huu.

KrishJenner ni mama wa watoto wafanyabiashara na wanamitindo maarufu KylieJenner, KimKardashian, KendallJenner, KhloéKardashian, #KourtneyKardashian, RobKardashian aliyowapata na marehemu mumewe RobertKardashian.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live