Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trela ya Game ya GTA 6 yavunja rekodi ya Dunia

GTA Trailer Trela ya Game ya GTA 6 yavunja rekodi ya Dunia

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ina siku tatu, tangu kuzinduliwa kwa kipande cha kwanza cha ujio wa game hiyo ambayo inatarajiwa kutoka 2024, imeshavunja rekodi tatu za dunia katika kitabu cha Guiness. Zaidi ya watazamaji milioni 104 wametazama video hii, na kutokana na ujio wa game hii kusubiriwa na watu wengi Duniani.

Sasa, Guinness World Records imetangaza rasmi kuwa trela rasmi la GTA 6 imevunja rekodi tatu tofauti katika muda mfupi

1) Trela la video game ambalo imeweza kutazamwa ndani ya masaa 24 ikiwa na watazamaji milioni 90, 490,421,491.

2) Video isiyo ya muziki ambayo imetazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Awali, nafasi hii ilikuwa inashikiliwa na MR. Beast kwa video yake ya Every Country On Earth Inapigana Kwa $250,000.

3) Trela la video game ambalo limepata likes nyingi zaidi ndani ya masaa 24. Unaambiwa katika muda huo imefanikiwa kupata takribani likes milioni 8.9. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live