Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trela ya Filamu ya "DeadPool" yavunja rekodi

Dead Pool Trela ya Filamu ya "DeadPool" yavunja rekodi

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kionjo (Trailer) cha ujio wa filamu mpya ya ‘‘Deadpool and Wolverine 3’ ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza Jumapili wakati wa Super Bowl, imevunja rekodi kwenye mtandao wa You Tube baada ya kutazamwa na zaidi ya watazamaji milioni 365 ndani ya saa 24.

Hapo awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiriwa na filamu ya ‘Spider-Man: No Way Home’ ambayo ilikuwa na zaidi ya watazamaji milioni 355.5 ndani ya 24 za kwa mwaka 2021.

‘Deadpool and Wolverine’ ambayo nayo imetengenezwa na kampuni ya #Marvel, inatarajiwa kuachiwa Julai 26 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live