Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Travis avunja rekodi ya mauzo Marekani

Travis Aachia Albamu Mpya Travis avunja rekodi ya mauzo Marekani

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Utopia" ya Travis Scott ndiyo albamu kubwa zaidi ya mwaka kwa maili baada ya kukaa kwenye nafasi ya juu kwenye Billboard 200 wiki tatu mfululizo ambapo punguzo la kina kwa Vinyl limesaidia kuiweka juu.

Travis alipata mauzo ya units 185K za albamu nchini Marekani pekee wiki iliyopita, na kufikisha jumla ya mauzo ya units zaidi ya 800K, hii ni takribani hadhi ya platinamu ndani ya mwezi mmoja tu.

Kati ya mauzo 185K, Travis ziliyouzwa wiki iliyopita, 93K kati yao zilitoka kwa mauzo ya rekodi ya "Utopia" ya vinyl, ambayo yalipunguzwa kutoka $ 50 hadi $ 5 kwa muda mfupi.

Licha ya malipo ya chini, "Utopia" sasa inashikilia rekodi ya wiki kubwa zaidi ya mauzo ya vinyl kwa albamu ya R&B/hip-hop au rap na inashika nafasi ya 10 bora ya mauzo ya vinyl kwa albamu yoyote ipo katika nafasi ya saba hii haijawahi kutokea tangu 1991.

Jitihada zote ngumu hazijamfanya Travis kuambulia patupu, ameonekana akifurahia mafanikio yake kwa likizo za kifahari, tutegemee kumuona anarudi kazini hivi karibuni maana UTOPIA bado inauza na lazima itampatia shows nyingi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live