Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Travis Scott na Drake wamefunguliwa kesi ya madai ya Tsh. Trilioni 1.7

Travis Scott Drake Travis Scott na Drake wamefunguliwa kesi ya madai ya Tsh. Trilioni 1.7

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mwonekano wa mambo, Travis Scott atakuwa akikabiliwa na matatizo ya kisheria kwa muda mrefu sana. Kadri siku zinavyosonga, rapa huyo aliyeteuliwa na kuwania tuzo za Grammy amebadilisha upepo kutoka kuwa mmoja wa wasanii wanaouzwa sana na wanaotafutwa sana kwenye tasnia hadi kufikia kutengwa na makampuni.

Kwa jumla, mpaka sasa watu 10 wamepoteza maisha kutokana na msongamano wa watu hatari katika tamasha la Astroworld lililofanyika wiki iliyopita na kusababisha maafa makubwa, na imeripotiwa kuwa mpaka sasa wengine 100 walijeruhiwa.

Waathiriwa ni pamoja na Axel Acosta mwenye umri wa miaka 21 ambaye alikufa katika tukio hilo la kusikitisha.

Mpaka kufikia wiki hii kuna kesi zaidi ya 1oo zilizofunguliwa dhidi ya Scott, Drake, Apple, na Live Nation wakitakiwa kuwalipa wahanga watukio hilo kiasi cha dola Milioni 750, na TMZ imedai kuwa idadi ya waathirriwa wanaotaka kupeleka kesi zaidi mahakamani imeongezeka.

Pesa hizo zinaripotiwa kugharamia matibabu, "majeraha ya kiafya na kiakili pamoja na kupoteza maisha." Wakati huo huo, wakili wa Scott ameiambia TMZ kwamba rapper huyo amejificha nyumbani kwake tangu mkasa huo na amekuwa akiwasiliana na familia zilizoathiriwa na tukio hilo baya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live