Tracy Edward; ni mtu pekee aliyefanikiwa kumtoroka muuaji Jeffrey Dahmer na kuwasaidia Polisi kumkamata baada ya kukutwa mtaani akikimbia na pingu mkononi mwake alijielezea na kuwaongoza Polisi kwa mtuhumiwa Jeffrey, Tracy Edward alikuwa anaenda kuwa kafara wa 18 kwenye orodha ya watu aliyowaua Jeffrey Dahmer.
Muathirika huyu alikutana na Jeffrey Dahmer katika klabu ya bia Julai 22,1991, ambapo walipewa ofa yeye pamoja na marafiki zake waliyomo wawili, Jeffrey Dahmer aliahidi kumlipa mtu yoyote kati yao dola 100$ ikiwa atakubali warudi nyumbani kwake na kupiga picha za uchi na hapo ndipo Tracy kuingia mtegoni na kuishia kuwa muathirika wa mwisho wa unyama wa Jeffrey Dahmer.
Ingawa Tracy alifanikiwa kukwepa kifo siku hiyo lakini maisha yake baada ya hapo yalikuwa ni ya kuhuzunisha sana, kwa mwaka 1992, alitoa ushuhuda wa kila kitu kwa undani zaidi kuhusu kilichomtokea katika usiku ule wa kutisha.
Kufikia mwaka 2002, Tracy Edward alikuwa akitanga tanga nyumba mpaka nyumba kwa kuwa aliishia kuwa masikini wa kutupa na toka hapo muathirika huyo aliyekwepa kifo alikuwa akijihusisha na madawa ya kulevya na wizi.
Kufikia mwaka 2011, ambapo Tracy Edward akiwa na miaka 52 alifanya mauaji ya kijana aliyeitwa Jonny Jordan kwa kumsukuma toka darajani na alikufa kabla ya waokoaji kuwahi kufika katika eneo hilo la tukio, Tracy alishtakiwa na kufungwa jela kwa muda wa mwaka mmoja na nusu baada ya hapo akawa chini ya usimamizi wa mahakama kwa miaka miwili.
Orodha ya watu waliouawa na Jeffrey Dahmer
Muuaji Jeffrey Dahmer alitoa uhai wa mtu wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 18 ambaye alisaga mifupa yake na kuisambaza kwenye uwanja wa nyumba aliyokuwa akiishi, alipoulizwa kwanini alifanya hivyo jibu lake Dahmer lilikuwa ni alihisi kutokwa na upweke kwa kuwa yule mtu aliyemuua alizunguka uwanja wa nyumba ile.
Monster of Milwaukee ni jina ambalo Jeffrey Dahmer alijiwania baada ya unyama alioufanya kwa kuua watu 17 ikiwemo kijana mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 14 tu alidondokea kuwa kafara kwa Jeffrey, akiwa jela alipokea zawadi na barua zilizohusisha pesa kwa watu waliokuwa wakijiita mashabiki zake na hiki kilimfurahisha sana Jeffrey.
Baada ya kutumikia miaka miwili jela Jeffrey alichomwa kisu na kuuwawa na mmoja wa wafungwa waliokuwa nae wakati tukio la mkanganyiko lilipotokea sehem ya kufulia nguo, Jeffrey alikuwa na Borderline Personality Disorder, Schizotypal Personality Disorder, na Psychotic Disorder.